Friday, May 15, 2015
Thursday, May 14, 2015
10:09 AM
MZM
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi wa shule za msingi za Mwangaza na Ngarenaro, juzi walidaiwa kupata kipigo kutoka kwa vijana waliojiita ‘Makamanda’ wa umoja wa vyama vya siasa vya upinzani ujulikanao kama Ukawa, baada ya baadhi yao kufika katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya karibu na shule yao.
Baadhi ya viongozi wakuu wa umoja huo, akiwemo mwanasheria wa
Chadema, Tundu Lissu, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
(NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless
Lema, walishuhudia kitendo hicho, lakini cha kushangaza hawakuchukua
hatua yoyote ya kuwazuia vijana hao kuwachapa watoto mijeledi kwa
kisingizio kuwa hawakustahili kuwepo uwanjani hapo.
Hatua hiyo imekuja licha ya kuwa umoja huo ulikuwa unafanya mkutano
wake katika eneo la shule ya Msingi Ngarenaro, uwanja ambao hutumika na
shule za msingi za Ngarenaro na Mwangaza pamoja na shule ya Sekondari ya
Ngarenaro.
Tuesday, May 12, 2015
6:14 AM
MZM
BEN POL KUJA NA REMIX YA SOPHIA KUTOKA CONGA MUSIC...
Waweza pia kucheki na kudownload video kutoka kitaa kwetu blog
Wednesday, May 6, 2015
7:51 AM
MZM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani vikali shambulizi
la waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo limeuwa
wanajeshi wawili wa umoja huo ambao wanatoka Tanzania.
Shambulizi hilo lilifanywa Jumanne jioni katika kijiji cha Kisiki,
umbali wa km 38 Kaskazini mwa mji wa Beni. Mbali na wanajeshi wawili
waliouawa na 13 ambao walijeruhiwa, wengine wapatao 4 hawajulikani
walipo.Wanajeshi wa Tanzania ambao ni sehemu ya kikosi maalumu cha kuingilia kati walikuwa wakifanya doria walipofanyiwa shambulizi hilo na watu wanaoaminika kuwa waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda.
Sunday, May 3, 2015
6:32 AM
MZM
Bomu lajeruhi watu watano mkoani Morogoro.
Bomu hilo liliwajeruhi watu hao walipokuwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Msolwa Ujamaa, Kata ya Sanje ,wilayani Kilombero, mkoani Morogoro
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:00 usiku wa Mei Mosi mwaka huu eneo la Kijiji cha Sanje.
Alisema vijana wawili wanaotuhumiwa kurusha mlipuko huo baada ya kuwajeruhi watu hao watano, walifanikiwa kukimbia kutoka eneo la tukio na jeshi la Polisi inaendelea kuwasaka ili sheria ichukue mkondo wake.
6:09 AM
MZM
Mwanamuziki Peter Okoye katika pozi
Hatua hiyo imepelekea Peter, kuweka wazi kuwa, kugombana kwao kusichukuliwe kama kitu cha ajabu kwani nao ni binadamu hivyo kukosana kupo na hakupingiki.
Amesema kuwa kutofautiana kwao ni jambo la kawaida na imekuwa ikitokea hivyo mara nyingi lakini baadaye maisha yanaendelea.
Ameongeza kuwa huwa inatokea kutofautiana kwa hapa na pale kama walivyo binadamu wengine na baadaye kumaliza tofauti zao na kufanya kazi.
Amesema kuwa wao ni kama wanandoa walioishi kwa zaidi ya miaka 20 hivyo kukosana kupo na kama binadamu hupatana na kupanda jukwaani kufanya makamuzi kama kawaida bila watu kujua kama wamegombana.
6:06 AM
MZM
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Weru Sengo anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Steve Nyerere, ambapo wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali wakila bata.
Inadaiwa kuwa badala ya kutoka katika matembezi au kula bata na mke wake, Steve, amekuwa akitoka na Weru, jambo ambalo watu wameona sio la kulifumbia macho na inadaiwa kuwa hata katika shoo ya Zari, walikuwa wote na kumuacha mke wake.
Vyanzo hivyo vimedai kuwa Steve, aweke bayana kama ameamua kuoa mke wa pili bila kumshirikisha mke wake kabla hawajamfanyia maandamano kama wanawake kutokana na mke wake kuwa mvumilivu na mtu anayejiheshimu.
Chanzo hicho kimetoa wito kwa mke wa Steve kumpenda mume wake zaidi ya mwanzo, kama amesikia au kuona kitu ni kawaida kwenye ndoa kupata majaribu, hivyo asimame kama mama na kudai kuwa lazima kama mke anajua udhaifu wa mume wake na kumtaka amkamatie hapo kwenye udhaifu bila kusahau kumuomba Mungu.
Kwa mujibu wa mke wa Steve, Suzy Cleo, amesema kuwa anashukuru kwa ushauri alioupata kutoka cha chanzo makini na kudai kuwa atahakikisha kuwa hatatikisika kama mwamba wa mlima Sayun
6:01 AM
MZM
Rio Ferdinand akiwa na mkwewake Rebecca Ellison enzi za uhai wake
Rebecca alizaa watoto watatu na Ferdinand, watoto wao wanafahamika kwa majina ya Lorenz, Tate na Tia.
Habari hizi zimemdhoofisha Ferdinand wakati huu mgumu wa ligi kuu ya soka Uingereza, Ferdinand kwa sasa anapambana kwenye kikosi chake cha Queens Park Rangers kuhakikisha kinasalia kwenye likgi kuu kwa msimu ujao.
5:18 AM
MZM
Tarehe May 1, 2015
Kuelekea pambano la ndondi la kukata na shoka kati ya Floyd
Mayweather Jr dhidi ya Manny Pacquiao ‘Pac Man’ kuna orodha ya mabondia
watano ambao kwa nyakati tofauti wamewahi kupambana na Mayweather na
Pacquiao.
Na hivi ndivyo namna ambavyo kila mmoja aliwashinda wapinzani hao.
OSCAR DE LA HOYA
Mayweather alishinda, ilikuwa ni mwaka 2007
Pacquiao alishinda, ilikuwa ni mwaka 2008
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mchezo huo wanasema kuwa, Pacquiao alishinda kwa mbinu bora zaidi.
Pacquiao (kushoto) akiwa na Mayweather na rekodi zaokwa pamoja
Na hivi ndivyo namna ambavyo kila mmoja aliwashinda wapinzani hao.
OSCAR DE LA HOYA
Mayweather alishinda, ilikuwa ni mwaka 2007
Pacquiao alishinda, ilikuwa ni mwaka 2008
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mchezo huo wanasema kuwa, Pacquiao alishinda kwa mbinu bora zaidi.
Floyd Mayweather akimchapa konde la maana usoni mpinzani wake Oscar de la Hoya
Manny Pacquiao akimchakaza pia De La Hoya na kumsababishia kustaafu masumbwi rasmi
RICKY HATTON
Mayweather alishinda kwa Techinical Knock Out mwaka 2007, tarehe 10
Pacquiao alishinda kwa Knock Out tarehe , 2009
Katika hili pambano Pacquiao anapewa faida kwa kushinda kwa ubora zaidi ya Mayweather
Hapa anasema; “Bado narudia kwa kusema kuwa Floyd anatakiwa kujifunza zaidi namna ya kumpiga huyu”, De La Hoya.
JUAN MANUEL MARQUEZ
Mayweather alishinda mwaka 2009
Pacquiao alidroo mwaka 2004
Pacquiao alishinda mwaka 2008
Pacquiao alishinda kwa pointi za majaji 2011
Pacquiao alipoteza kwa Knock Out katika raundi ya 6 mwka 2012
Hapa karata imemuangukia Mayweather.
SHANE MOSLEY
Mayweather alishinda mwaka 2010
Pacquiao alishinda mwaka 2011
MIGUEL COTTO
Mayweather alishinda mwaka 2012
Pacquiao alishinda mwaka 2009
Mayweather vs Pacquiao: kwenye pambano hili Pacquiao alionekana kushinda kwa mbinu bora zaidi ya Mayweather.
Miguel anasema: “Manny ana kasi na nguvu. Manny yuko bora zaidi ya Mayweather”
Mayweather alishinda kwa Techinical Knock Out mwaka 2007, tarehe 10
Pacquiao alishinda kwa Knock Out tarehe , 2009
Katika hili pambano Pacquiao anapewa faida kwa kushinda kwa ubora zaidi ya Mayweather
Hapa anasema; “Bado narudia kwa kusema kuwa Floyd anatakiwa kujifunza zaidi namna ya kumpiga huyu”, De La Hoya.
Mayweather akipambana na Ricky Hatton
Pacquiao akionekana kumchakaza Ricky Hatton kiasi cha kupoteza fahamu kabisa katika mzunguko wa pili tu
Mayweather alishinda mwaka 2009
Pacquiao alidroo mwaka 2004
Pacquiao alishinda mwaka 2008
Pacquiao alishinda kwa pointi za majaji 2011
Pacquiao alipoteza kwa Knock Out katika raundi ya 6 mwka 2012
Hapa karata imemuangukia Mayweather.
Mayweather akipambana na Manuel Marquez
Marquez alimpa Pacquiao wakati mgumu sana, lakini alisubiri mpaka pambano la mwisho kati ya mapambano 4 kumshinda Pacquiao
Mayweather alishinda mwaka 2010
Pacquiao alishinda mwaka 2011
Mayweather akimuadhibu Mosley
Mosley akipokea kichapo toka kwa Pacquiao
Mayweather alishinda mwaka 2012
Pacquiao alishinda mwaka 2009
Mayweather vs Pacquiao: kwenye pambano hili Pacquiao alionekana kushinda kwa mbinu bora zaidi ya Mayweather.
Miguel anasema: “Manny ana kasi na nguvu. Manny yuko bora zaidi ya Mayweather”
Miguel Cotto akimtundika konde Mayweather kabla ya kushindwa katika raundi ya mwisho kabisa ya mchezo
Pacquiao akizichapa dhidi ya Cotto
Saturday, May 2, 2015
8:24 AM
MZM
![]() |
| KWANZA KABISA WANAANZA TOA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA NA KUZANIWA AMEROGWA NA ALIYEZIKWA AKIWA HAI MAANA KATIKA KABURI HILO WALIZIWA WATU WAWILI KATIKA KABURI MOJA ALIE HAI NA MFU |
![]() |
| JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA TAYARI LIMETOLEWA HILO PEMBENI SASA ANAFUKULIWAALIEZIKWA HAI |
![]() |
| MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI SASA UNATOLEWA KABURINI |
7:21 AM
MZM
- Ujerumani imetuma meli mbili za jeshi lake la wanamaji katika juhudi za kuokowa wakimbizi wasipoteze maisha yao katika bahari ya Mediterenia wakati wakikimbilia barani Ulaya kutafuta maisha bora.
-
- Meli ya kivita ya usaidizi "Berlin" na manowari "Hessen" za Ujerumani.
- Meli hizo mbili meli ya kivita ya usaidizi yenye jina la Berlin na manowari inayoitwa Hessen zimeondoka hapo Ijumaa (1.05.2015) katika eneo la Pembe ya Afrika kwa kupitia Mfereji wa Suez nchini Misri kabla ya kuingia bahari ya Mediterenia.
- Msemaji wa jeshi la wanamaji la Ujerumani mjini Rostock ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba meli hizo mbili ilikuwa zinatarajiwa kutia nanga huko Souda katika kisiwa cha Ugiriki cha Crete hapo Jumamosi(02.05.2015).
- Amesema meli hizo zitatumika kusafrisha chakula na mablanketi kwa ajili ya wakimbizi wanaohatarisha maisha kukimbilia Ulaya kwa kupitia bahari ya Mediterenia ambapo wiki chache zilizopita mashua moja iliokuwa imebeba wahamiaji kutoka Libya ilizama na kuuwa takriban watu 800.
Friday, May 1, 2015
9:26 AM
MZM
Saudi Arabia imesema majeshi yake yamewauwa na waasi wa Yemen waliofanya
shambulizi lao la kwanza kubwa dhidi ya nchi hiyo tangu kuanza mwezi
uliopita mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Saudia
Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema wanajeshi wake watatu pia
waliuawa katika mapambano hayo baada ya waasi wa Houthi kuvilenga vituo
vyao vya uangalizi, wakati jeshi lake likijaribu kuzuia shambulizi hilo.
Kumekuwa na makabiliano hapo kabla lakini hii ni mara ya kwanza ambapo
jeshi la Saudi Arabia limeripoti kuhusu shambulizi kamili la waasi wa
Houthi katika mipaka yake. Katika mji mkuu Sanaa, mashambulizi mapya ya
kutokea angani yanayoongozwa na Saudia yamefanywa katika uwanja wa ndege
ikiwa ni siku chache tu baada ya ndege za kivita kuilipua njia ya ndege
katika uwanja huo ili kuzuia ndege moja ya Iran kutua.
Wakati huo huo, mawaziri wa mataifa ya Ghuba hapo jana walipinga
pendekezo la kuandaa mazungumzo katika nchi isiyounga mkono upande
wowote katika mzozo wa kisiasa nchini Yemen, wakati ripoti ya watalaamu
ikisema kuwa Iran imekuwa ikiwapa silaha waasi wa Houthi tangu mwaka wa
2009.
Wednesday, April 29, 2015
9:32 AM
MZM
Indonesia imewauwa wasafirishaji nane wa madawa ya kulevya siku ya
Jumatano, wakiwemo raia saba wa kigeni, hatua iliyolaaniwa vika nya
Australia na Brazil, zilizojaribu kuwaokoa raia wake bila mafanikio.
Australia ilimuondoa balozi wake kutoka Indonesia kupinga mauaji hayo yaliyofanyika saa sita za usiku, lakini rais wa Indonesia Joko Widodo amesema alikuwa akitekeleza tu sheria dhidi ya wasafirishaji wa madawa ya kulevya.
Watuhumiwa hao -- wawili kutoka Australia, moja kutoka Brazil na wanne kutoka Nigeria -- waliuawa kwa kupigwa risasi pamoja na Muindonesia moja, licha ya kelele za mataifa ya kigeni na maombi ya huruma kutoka kwa wanafamilia wao.
8:36 AM
MZM
Maelfu ya maafisa wa polisi nchini Marekani wameamriwa kuwasaidia
maafisa waliozingirwa mjini Baltimore, baada ya ghasia zilizosababishwa
na waandamanaji waliojawa na hasira, kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi.
Muandamanaji akiwafokea polisi waliokuwa wanajaribu kudhibiti hali mjini Baltimore
Watu 27 wametiwa nguvuni huku polisi 15 wakijeruhiwa wakati waandamanaji
hao wengi wao wanafunzi waliokuwa wanarusha mawe na kupora biashara za
watu, walipopambana na maafisa wa polisi. Ghasia mjini Baltimore zilianza baada ya mazishi ya kijana Mmarekani mweusi kwa jina Freddie Gray, aliyekuwa na miaka 25 na aliyefariki tarehe 19 mwezi wa Aprili kufuatia majeraha mabaya ya uti wa mgongo aliyoyapata wakati alipokuwa anatiwa nguvuni na maafisa wa polisi.
8:17 AM
MZM
Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress ANC
kimelaani wimbi la mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni ambayo
yamesababisha vifo vya watu sita na kusababisha hali ya wasiwasi nchini
humo
ANC imeyataja mashambulizi hayo vitendo vya kihalifu dhidi ya watu wanyonge ambao wanatafuta hifadhi, faraja na kujiendeleza kiuchumi na kuongeza raia wa kigeni hapaswi kulaumiwa kwa changamoto zinazowakumba raia wa Afrika Kusini.
Katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Durban mashambulizi yaliyochochewa na chuki dhidi ya wageni yamezilenga biashara na makaazi ya raia wa kigeni wakiwemo kutoka Somalia, Ethiopia na Malawi licha ya polisi kuimarisha doria katika mji huo kuzuia mashambulizi hayo.
Rais yuko kimya
Taarifa hiyo kutoka kwa ANC inakuja baada ya shutuma kuwa Rais Jacob Zuma ameshindwa kutoa tamko hadharani kuyalaani mashambulizi hayo. Mapema mwaka huu, raia wa kigeni pia walishambuliwa na maduka yao kuporwa katika kitongoji cha Soweto kilichoko karibu na mji wa Johannesburg.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Mashirika ya kutoa misaada yamesema zaidi ya raia 2,000 wa kigeni
wameutoroka mji wa Durban wakihofia maisha yao na sasa wanaishi katika
kambi za muda chini ya ulinzi wa polisi na iwapo mashambulizi hayo
hayatasitishwa,idadi ya waathiriwa inatarajiwa kuongezeka.Mhamiaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Johnny ambaye ni raia wa Zimbabwe anasema anatafakari kurejea nyumbani
Jana maduka mengi yalifungwa katikati mwa mji wa Johannesburg baada ya wafanyaibishara kuhofia ghasia zitazuka baada ya vitisho kusambazwa katika mitandao ya kijamii.
Msumbiji imetangaza inapanga kuwasaidia raia wake walioko Afrika Kusini kurejea nyumbani baada ya waziri wa habari wa Malawi Kondwani Nankhumwa kusema wanawarejsha nyumbani raia wao 400 waliochomewa nyumba na mali zao. Malawi ndiyo nchi ya kwanza ya Afrika kuwaondoa raia wake kutoka Afrika Kusini.
Mfalme anashutumiwa kuchochea chuki
Mfalme Goodwill Zwelithini kiongozi wa kabila kubwa zaidi nchini Afrika Kusini la kwa Zulu Natal anashutumiwa kwa kuchochea mashambulizi hayo baada ya kutoa hotuba wiki mbili zilizopita akiwataka raia wa kigeni kufunga virago na kurejea makwao.
Baadhi ya waafrika Kusini wakikabiliana na raia wa kigeni mjini Durban
Mwakilishi wa mfalme huyo Thulani Zulu amekanusha kuwa mfalme huyo ndiye
aliyechochea mashambulizi hayo na kuongeza kuwa amesikitishwa na
yanayojiri na anayalaani .Wanaharakati wanaopinga chuki dhidi ya raia wa kigeni wanapanga maandamano makubwa mjini Durban hii leo kuishinikiza serikali kuchukua hatua zaidi kuwalinda wahamiaji. Polisi Afrika Kusini imesema imewakamata watu74 kuhusiana na mashambulizi hayo.
Raia wa Afrika Kusini ambao hawana ajira wanawashutumu wageni kuwa wanachukua nafasi zao za kazi. Mwaka 2008, watu 62 waliuawa katika mitaa ya Johannesburg kutokana na chuki hizo dhidi ya wageni.
8:10 AM
MZM
Juhudi za kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini
Tanzania zinapata nguvu mpya kupitia kampeni mbalimbali zinazolenga
kuhamasisha jamii kupinga vitendo hivyo vya kinyama.
Pamoja na kampeni kadhaa zilizoanzishwa, siku ya Jumapili (tarehe 15
Machi) kulitarajiwa kuzinduliwa kampeni nyingine inayotumia kombe
maalumu litakalozungushwa nchini kote kutuma ujumbe wa amani na kupinga
mauaji ya albino.Kampeni hii inazinduliwa katika wakati ambapo jeshi la polisi likitangaza kuwatia mbaroni zaidi wa waganga wa kienyeji 55 wanaotuhumiwa kupiga ramli zinazochonganisha watu ikiwamo zile zinazochochea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Tuesday, April 21, 2015
6:29 AM
MZM
Serikali imerejesha mafunzo ya madereva kila baada ya miaka mitatu wakati wa kumalizika kwa muda wa leseni zao, huku ikifafanua kuwa elimu watakayoipata ina umuhimu katika kazi zao, kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika sekta hiyo.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, alitangaza uamuzi huo wa
Serikali jana katika mkutano kati yake na viongozi wa madereva wa mabasi
nchini.
Mkutano
huo umefanyika kama ilivyoahidiwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia
Kabaka, wakati alipokuwa akijitahidi kumaliza mgomo wa madereva
uliofanyika Aprili 10 mwaka huu, wakati walipokuwa wakipinga pamoja na
mambo mengine, sharti la kwenda shule ili kupata leseni mpya.
Madereva
hao walitaka Serikali ifanyie marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani,
kwa kuondoa kipengele kinachowataka madereva kwenda Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) kwa mafunzo ya muda mfupi kila wakati leseni zao
zinapoisha, ili kupata sifa ya kupata leseni nyingine.
Sababu
ya kupinga kupata mafunzo, ilidaiwa kuwa utaratibu huo uliotangazwa
Machi 30, mwaka huu, ulianzishwa bila kushirikisha madereva katika
kuuandaa.
Pia
walipinga kutakiwa kujilipia gharama za shule hiyo ambazo walidai ni Sh
560,000 kwa magari ya kawaida na Sh 200,000 kwa magari ya abiria.
Sababu
nyingine iliyochangia wapinge shule hiyo, walidai ni kukosekana kwa
mikataba ya ajira, inayoweza kuwahakikishia kulindwa kwa kazi zao hadi
wanapomaliza mafunzo.
Madai
mengine yaliyokuwa nje ya shule hiyo, madereva hao walitaka kuondolewa
kwa faini ya Sh 300,000 kwa kila kosa la barabarani na kuitaka Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra), kuhakiki
uhalisia wa dereva anayeandikishwa na mmiliki wa chombo husika.
Majibu
ya Serikali Mahanga aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alisoma tamko
la Serikali lililoeleza kuwa pamoja na kurejesha mafunzo hayo,
utekelezaji wake hautafanyika mara moja kwa kuwa Kanuni zake
hazijakamilika.
“Tangazo
hili (la kwenda shule) limetolewa kwa kuzingatia umuhimu wa mafunzo
kazini kwa wafanyakazi na madereva kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine,”
alisema Mahanga.
Alisisitiza
kuwa baada ya miaka mitatu ya leseni, dereva atatakiwa kupata mafunzo
mafupi, ambayo ni kati ya siku tatu hadi saba na atakayegharimia mafunzo
hayo ni mwajiri, si mfanyakazi na ni katika chuo chochote
kinachotambulika.
Akifafanua,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwamini Malemi aliyekuwepo
katika mkutano huo, alisema mitaala ya mafunzo hayo bado inaandaliwa,
hivyo si rahisi Kanuni hiyo kuanza kutekelezwa mwaka huu hata kama
zitakamilika.
Kuhusu
mikataba ya ajira ambayo ililalamikiwa mno na madereva wakati wa mgomo,
Mahanga alisema Serikali itapitia upya mikataba hiyo ili kuhakikisha
mambo yote muhimu yanazingatiwa.
Akiongezea
hoja katika suala la mikataba, Malemi alisema ni lazima mikataba iwe
imekamilika kabla ya kuanza kutumika kwa kanuni ya kwenda shule, ili
ioneshe wajibu wa mwajiri katika kumsomesha mfanyakazi.
Kuhusu
kauli iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova ya kuondoa tochi za kupima mwendo kasi barabarani, Mahanga
alisema matumizi ya tochi zinazotumika kupima mwendo kasi na ratiba ni
sehemu ya utekelezaji wa Sheria za Usalama Barabarani.
Hoja
nyingine Katika kikao hicho mbali na hoja zilizosababisha mgomo,
kulikuwa na hoja nyingine zilizowasilishwa, ikiwemo changamoto ya
madereva kupata maelekezo yanayokinzana kutoka Jeshi la Polisi na
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra), kuhusu
ratiba ya kuondoka wanakotoka na kuwasili wanakokwenda.
Akitoa
majibu ya Serikali, Mahanga alisema amepokea hoja hiyo na ataifanya
utafiti wa kina. Katika hoja ya kuwataka waajiri kuongeza posho za kazi,
Mahanga alisema Serikali haiwezi kupanga posho za madereva katika kikao
hicho, kwasababu kila mwajiri ana uwezo wake kulingana na safari za
gari yake.
Hata
hivyo, aliahidi kufanyika utafiti suala hilo katika nchi nyingine, ili
aone namna ambavyo madereva wengine wamekuwa wakilipwa posho.
Serikali
pia imeahidi kuimarisha ukaguzi sehemu za kazi kwa kushirikiana na
Sumatra, utakaohusu wamiliki wa magari na kuhuisha mfumo wa kumbukumbu,
utakaoonesha kila gari na dereva wake halisi na kuweka vitambulisho vya
dereva katika kila gari analoendesha.
Mahanga
alisema Serikali pia itaweka utaratibu mpya ambapo dereva mwenyewe
atajiwekea bima ya ajali itakayoanzishwa na kujiunga na vyama vya
wafanyakazi, ili watetee mikataba yao ili iweke pia maswala ya bima
hizo.
Alisema pia Serikali imeanzisha Mfuko wa Fidia ya Wafanyakazi, ambao utaanza hivi karibuni, ambao mwajiri atawajibika kuchangia.
Chama cha Wafanyakazi
Kuhusu
chama cha wafanyakazi, Mahanga alisema Serikali imepokea pendekezo la
kusaidia madereva kuunda chama cha wafanyakazi chenye nguvu, ambapo
alisema kumbukumbu zinaonesha madereva wana vyama vilivyosajiliwa kwa
Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri.
Alitaja
vyama hivyo kuwa ni Umoja wa Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafiri
Tanzania (COTWU), kilichosajiliwa mwaka 2000 na Chama cha Wafanyakazi
cha Usafiri wa Barabara (TARWORTU) kilichosajiliwa mwaka 2013.
“Katika
kushughulikia changamoto za wafanyakazi na mwajiri wote mnategemeana,
jambo mtakalofanya ni kuanzisha majadiliano kupitia vyama vya
wafanyakazi lakini kwanza muwe ndani ya vyama,” alisema Mahanga.
Wanung’unika
Baada
ya kusomwa kwa tamko hilo la Serikali, Katibu Mkuu wa Vyama vya
Madereva Tanzania, Mwanarashidi Salehe, alisema mafunzo wanayotakiwa
kuchukua hayana tija yoyote, kwa kuwa wakufunzi ni wa kizamani na pia
magari yanayotumika ni ya kizamani, ambayo hayaongezi chochote katika
kazi yao.
“Kwanza
hakuna kipya katika mafunzo hayo, mimi nimehudhuria mara mbili....pili
katika kikao hiki tulitarajia tutakutana na wamiliki wa magari ambao
ndio waajiri wetu ili waseme waliyonayo juu yetu na sisi tuseme yetu
tujadiliane na kupata majibu,” alisema Salehe.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Clement Masanja alisema mikataba waliyonayo madereva ni
dhaifu mno, haioneshi mambo ambayo dereva atanufaika nayo.
“Tulitarajia
katika kikao hiki tutatoka na majibu ya posho za madereva, ili dereva
ajue atalipwa kiasi gani kwa safari za ndani na nje ya nchi kwa sababu
anavyolipwa ni manyanyaso matupu,” alisema Masanja.
Sunday, April 19, 2015
2:53 AM
MZM
wewe
ni dereva wa basi la abiria ama gari binafsi ?hebu chukua hatua
ya kupunguza ajali leo kwa kujihadhari na kona hizi na Iyovi na
Kitonga na kona nyingine kali kama hizi nchini kwani maisha yako ni
dhamani kubwa na uhai wake bado tunautamani
Katika kona kama hizi zingatia alama za usalama barabarani usiwe na haraka ya kulipita gari la mbele
Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter






























