Sunday, June 26, 2016

 Sanamu (5)
Historia ya Mnara ule ilianza mwaka 1889, kisha, kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 - 1945).
Kwa ufupi Sanamu ya mwanzo kukaa pale ni sanamu ya Herman Von Wissman, Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir Ibn Salim Al Harthi, mtawala/sultani
wa Pangani Tanga.
June 24 2016 Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ‘TAMISEMI’ imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali, Kwa urahisi zaidi unaweza kuyaona majina yote kwenye hii link hapa

Friday, June 17, 2016


Rapper Chidi Benz amefanikiwa kuirudisha afya yake baada ya kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.

Mapema mwaka huu katika kituo kimoja cha runinga Chidi Benz alikiri kutumia Madawa ya kulevya na kuomba msaada ambapo meneja Diamond na Tip Top Connection, Babu Tale akishirikiana na Kalapina walimsaidia na kumpeleka katika kituo cha Bagamoyo Sober House ambacho kilimsaidia kuachana na Matumizi ya madawa ya kulevya.

Wednesday, June 8, 2016


Nchini kenya waziri wa fedha Henry Rotich leo amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya matumizi ya pesa za serikali katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Bajeti hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo. Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.
Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.
Kama ilivyo ada bajeti inaposomwa kuna wale wa wanaofaidi na wale wanaopoteza. Gesi ya kupikia na chakula cha mifugo umeondolewa ushuru, Huku ushuru wa petroli na mafuta taa ukiongezwa. Bidhaa za mafuta ya urembo zikiwekewa ushuru wa asilimia kumi kwa mara ya kwanza.
Waziri ametenga shilingi bilioni 4.3 kwa huduma za bure za wanawake wajawazito kujifungua,milioni 19.7 kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 na shilingi milioni 7.9 kwa watoto mayatima.


Nchini Tanzania makadirio ya bajeti ya mwaka 2016 na 2017 ni trilioni 29,5 pesa za Tanzania ikiizidi bajeti ya mwaka wa 2015 na 2016 kwa trilioni 7.1.
Waziri wa Fedha nchini Tanzania Phillip Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 18.46 zitatokana na jumla ya mapato ya ndani.
Kiwango hicho kimezidi shilingi trilioni 3.64 za bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya shilingi trilioni 4.82.
Shilingi trilioni 17.72 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zikitengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Bwana Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.88 zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.
Makadirio ya bajeti nchini Uganda mwaka 2016 na 2017 iliyosomwa leo ni ya jumla ya dola bilion 7.5 ambayo ni sawa na trillioni 27. 3 pesa za Uganda, tofauti na bajeti ya mwaka uliopita ya mwaka 2015 na 2016 ambayo ilikuwa ni dola bilioni 6.9.
Bajei kubwa mwaka huu nchini Uganda imeelekezwa kwa wizara ya kazi na uchukuzi ambayo ilipewa dola blioni 1.1 huku wizara ya ulinzia ikipewa dola milioni 435. Wizara ya afya imepata dola milioni 525.
Wizara ya nishati na maendeleo ya madini ilipata dola milioni 695 huku Wizara ya kilimo ambayo nidiyo muhimu nchi Uganda ikiewa dola milioni 522.

Tuesday, May 31, 2016

Msanii Korede Bello aachia wimbo wake mpya unaoitwa One and Only kama video yake inavyoonekana hapojuu.unaweza kuiangalia moja kwa moja hapo juu

Monday, May 30, 2016

 
Chuo kikuu cha Dodoma
Wanafunzi katika chuo kikuu cha Dodoma nchini Tanzania wamefukuzwa chuoni humo baada ya kuzuka kwa mgogoro kati ya serikali na wahadhiri wa chuo hicho.
Wanafunzi hao waliagizwa kuondoka katika chuo hicho kufikia saa kumi na mbili jioni siku ya Jumapili.

Ilani
Ilani hiyo imesema kuwa kulikuwa na makosa katika mafunzo ya wanafunzi wanaosomea shahada ya elimu ikiwemo sayansi,hesabati,teknolojia hivyobasi serikali imewataka wanafaunzi hao kuondoka chuoni humo hadi ilani nyengine itakapotolewa.
Maelezo kuhusu mgogoro huo kati ya wahadhiri wa chuo hicho na serikali hayajulikani.

Thursday, May 26, 2016

Wolper akiri kuwa na uhusiano na Harmonize, asema hakujua kama ‘Mkongo’ ana mke.
Mwigizaji Jackline Wolper jana amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin ‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.
‘Ni kweli Raj (Harmonize)ni mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.

Tuesday, May 24, 2016


3ede2cfb-a205-4083-9c8e-b5227c971c2b

Zitto Kabwe akimvisha pete mchumba wake
Zitto Kabwe amemchumbia msichana mrembo anayetarajia kumbadilisha jina soon kuwa ‘Mrs Kabwe.’ Mchumba wake anaitwa Anna Bwana anayefanya kazi BBC Media Fund ambapo kabla ya hapo alikuwa mfanyakazi wa shirika la Oxfam.
Baada ya kuwasaini Davido na Alikiba, record label kongwe duniani, Sony Music imemsaini msanii wa Afrika Kusini, Mobi Dixon.
Mobi-Dixon
Mobi Dixon anakuwa msanii wa tatu kutoka Afrika kusainiwa kwenye label hiyo.

Monday, May 23, 2016


Kialama cha WhatsApp
WhatsApp imepitia mabadiliko mengi, na imekuwa kati ya applications zinazotumika na kupendwa zaidi duniani. Baada ya kununuliwa na Facebook, waendelezaji walianza kuongeza vitu vipya kama kupiga simu za sauti, kuweza kutuma mafaili, na kuongezwa kwa usalama zaidi. Kwasasa, WhatsApp ni moja kati ya application yenye watumiaji wengi zaidi, ikiwa na angalau watumiaji bilioni moja wanaotumia kikamilifu kila mwezi. Katika makala hii, tutafahamisha baadhi ya vitu vilivyopo WhatsApp na havitumiki mara nyingi, na namna vinavyoweza kutumika;

Saturday, May 21, 2016

Msanii Kadjanito ameachia video mpya ya wimbo ‘One More Night. Video imeongozwa na GQ Digital Vibes.
Msanii wa Hip Hop Stamina ameachia wimbo mpya unaitwa “Mmeniroga”, Producer Rash Don

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

Friday, May 20, 2016

Swala
Shambulio lilitekelezwa wakati wa swala jioni
Polisi nchini Tanzania wanawazuilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika shambulio katika msikiti mmoja mjini Mwanza magharibi mwa nchi hiyo.
Watu watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi jijini humo, Ahmed Msangi, uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia mapanga na kuongeza kuwa, polisi wanachunguza chanzo cha shambulizi hilo.
Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, wamesema shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wasiopungua 15.
Staa wa Marekani, Ne-Yo jana usiku alitua jijini Dar es Salaam akitokea Marekani akiwa na ulinzi mkali.
Muimbaji huyo wa ‘Miss Independent’ alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mida ya saa tano kasoro usiku. Staa huyo aliyekuwa amevaa nguo zote nyeusi na kofia ambayo alikuwa ameifunika na hood aliwapungia mkono waandishi wa habari na mashabiki waliokuwa wamejitokeza kumpokea kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye gari na kufunga vioo.
Mlinzi wake pandikizi la mtu, alimzuia staa huyo kutoongea na waandishi wa habari kwa kudai kuwa alihitaji kupumzika kutokana na uchovu wa safari hiyo. Hata hivyo baada ya kuombwa na waandishi wa habari walau wamuulize maswali machache, alifungua kioo cha gari na Ne-Yo kusalimia.
“Fantastic so far,” alijibu Ne-Yo baada ya kuulizwa anajisikiaje kuja Tanzania. “ I am happy to be here looking forward to perform with Diamond and everyone who will be at the show,” aliongeza.
Ne-Yo atatumbuiza Jumamosi hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka linalodhaminiwa na Vodacom. Diamond na wasanii wengine zaidi ya 20 watatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM.
Drake amezidi kuonyesha ubora wake kwenye tuzo za BET zitakazofanyika, Juni 26 huko Los Angeles, Marekani.
drake
Mwaka 2016 umekuwa wa neema kwa Drake baada ya kuonekana mara tisa kati ya vipengele sita alivyowekwa akifuatiwa na Beyonce pamoja na Rihanna. Pia albamu yake ya ‘Views’ inazidi kushika namba moja kwenye chati za Billboard baada ya kuuza nakala zaidi ya milioni 1.04 ndani ya wiki mbili tangu alipoiachia mwishoni mwa mwezi Aprili.
Tuzo hizo za BET zitafanyika kwenye ukumbi wa Microsoft Theater, Los Angeles huku Afrika Mashariki tukiwakilishwa na Diamond kwenye kipengele cha Best International Act: Africa lakini pia atafanikiwa kufanya show kwenye tuzo hizo.

Wednesday, May 4, 2016

 Jani
Mvulana huyo amepewa $10,000
Mvulana wa umri wa miaka 10 nchini Finland ameshangaza wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mvulana huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua udhaifu huo uliowezesha mtu kuingia kwenye mtandao huo wa kusambaza picha na kufuta maoni ya watu.
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kisheria haruhusiwi kutumia mtandao huo hadi atimize umri wa miaka 13.
Facebook, inayomiliki Instagram, ilichukua hatua upesi na kuondoa udhaifu huo.
Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo.
Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.
Wataalamu wa mtandao huo walimfungulia akaunti ndipo aweze kuthibitisha madai yake na akafanikiwa.
Mvulana huyo kutoka Helsinki, ameambia gazeti la Iltalehti la Finland kwamba atatumia pesa hizo kununua baiskeli, mpira na mavazi ya kuchezea kandanda na kompyuta za kutumiwa na ndugu zake.

Facebook imeambia BBC kwamba imelipa jumla ya $4.3m kwa watu waliogundua udhaifu kwenye mitandao yake.
Malipo hayo hutolewa kama kishawishi kuzuia watu kuuzia wahalifu ugunduzi wao na hivyo kusaidia kampuni husika.
Bagaza
Kanali Bagaza alikuwa na umri wa miaka 69
Rais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji.
Kanali Bagaza amekuwa akitibiwa kwa muda katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels.
"Imethibitishwa, rais wa zamani Jean Baptiste Bagaza amefariki dunia akiwa nchini Ubelgiji,2 ameandika mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kwenye Twitter.
"Alikuwa seneta maisha.”
Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu wake Meja Pierre Buyoya Septemba 1987.

Tuesday, May 3, 2016


Afeni Shakur
Mamaake aliyekuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap Tupac Shakur ,Afeni Shakur amefariki akiwa na umri wa miaka 69.
Kaunti ya California imethibitisha kifo chake kupitia ujumbe wa Twitter.Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.
Alice Faye Williams,alibadilisha jina lake na kuitwa Shakur akiwa mtu mzima alipokuwa mwanaharakati wa kisiasa na kujiunga na vuguvugu la Black Panther.
Alikuwa na mimba ya Tupac mwaka 1971 alipokamatwa na kufungwa jela pamoja na wanachama wengine wa vuguvugu hilo na kukabiliwa na mashtaka ya njama ambayo baadaye yalitupiliwa mbali.
Shakur alikuwa kigezo kizuri cha muziki wa mwanawe na alisimamia muziko wake baada ya kifo chake.

 Tupac Shakur
Tupac Shakur alifariki mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25,baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika gari moja.
Mauaji yake bado hayajapata ufafanuzi.