Wednesday, January 10, 2018


Moto  mkubwa wa gesi umelipuka na kuteketeza nyumba eneo la Hospitali ya Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam jana jioni  kutokana na Bomba la gesi kutoka Songo Songo, Lindi/Mtwara kwenda Ubungo, Dar, kupasuka na kusababisha moto mkubwa uliozua taharuki kwa wakazi na wafanyabiashara wanaozunguka eneo la Buguruni Mnyamani.

Taarifa za awali za zilisema bomba hilo lililipuka baada ya mafundi wa Dawasco waliokuwa wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao ya maji, kulitoboa bomba hilo la gesi kimakosa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Benedict Kitalika, amesema  kwamba mafundi hao walikuwa wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao, na ndipo wakatoboa bomba hilo kimakosa.

Kamanda Kitalika ameendelea kwa kusema kwamba wameshawasiliana na watu wa Mtwara na kufunga bomba hilo, ili kupunguza kasi ya gesi.

Madhara yaliyosabaishwa na moto huo ni kuteketea kwa baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara, kuungua kwa nguzo za Tanesco na nyumba moja imeteketea kabisa lakini hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki dunia wala kujeruhiwa kutokana na moto huo.

0 comments: