Sunday, July 31, 2016


Msanii wa Nigeria "Tiwa Savage" aachiwa wimbo wake mpya "Bad" akimshirikisha "Wizkid". Video imefanywa na Director "Sesan"

Friday, July 22, 2016

Tume ya vyuo vikuu nchini TCU, imevizuia vyuo sita nchini kufanya udahili wa wanafunzi kwenye msimu wa masomo wa 2016/17.
WAZIRI-WA-ELIMU
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako (Kulia)

Hatua hiyo imechukuliwa na tume hiyo kutokana na vyuo hivyo kutokidhi viwango vya elimu vilivyokuwa vikiitoa.
Vyuo hivyo ni pamoja na:
1. International Medical and Technological University (IMTU) – all programmes.
2. St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS) – all programmes.
3. University of Bagamoyo (UoB) – all programmes.
4. St. Joseph University College of Engineering (SJUCET) – all programmes.
5. University of Dodoma (UDOM) – Doctor of Medicine Programme
6. State University of Zanzibar (SUZA). – Doctor of Medicine Programme.
Mchekeshaji Ismail Issa Makombe ‘Kundambanda’ amefariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa hii baada ya kusumbuliwa na matatizo ya tumbo kwa muda mrefu.
p.txt
Mwigizaji huyo ambaye pia aligombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwao Mtwara.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Mwenyekiti wa Chama cha wasanii wa Vichekesho Tanzania, Mkono Wa Mkonole amethitisha kutokea kwa msiba huo.
“Kweli ndugu yetu ametutoka na kwa taarifa zisizo rasmi kesho wanazika, lakini sisi kama wasanii wa vichekesho leo jioni tunakutana na kupanga jinsi ya kuweza kuhudhuria mazishi ya ndugu yetu,” alisema Mkonole.

Tuesday, July 12, 2016

Kama wewe ni mpenzi wa mziki mtamu kutoka Afrika basi huwezi kuchelewa kuiona video hii. Kwa hapa nadhani ni mwendo wa tuzo tu zinangojea kumiminika.
Basi ruka kidogoooooo.....

Saturday, July 2, 2016

 
Mkhitaryan
Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan amesajiliwa na klabu ya Manchester United ,kulingana na klabu hiyo ya Ujerumani.
Afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa msimu ujao.
''Iwapo tungekataa mchezaji huyo angekuwa huru mwaka 2017'' ,Watzke aliambia mtandao wa Dortmund.
United tayari imewasajili wachezaji wawili msimu huu akiwemo beki Eric Baily na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.