Friday, January 20, 2017

Wednesday, January 18, 2017

Watafiti wafanikiwa kutengeneza betri la simu aina ya lithium-ion lenye uwezo wa kuzima moto kama kama betri la simu likitaka kuungua – hili litaepusha milipuko ya mabetri.

Kemikali zinazohusika na kuzuia moto wa aina yeyote, (flame retardant triphenyl phosphate), zimewekwa sambamba na mjumuiko wa kemikali zinazohifadhi chaji, electrolyte fluid, ndani ya betri. Kwa namna yeyote ile kama joto katika mjumuiko huo wa electrolyte utafika nyuzi 150 za Sentigredi au zaidi basi kemikali za kuzuia moto zitaachiwa ndani ya betri husika na kuzima uwezekano wowote wa moto au mlipuko wa betri.
Majaribio yameonyesha mototo wowote ambao wataka katika betri hizo utaweza kuzimwa ndani ya sekunde 0.4.
Teknolojia hii (betri zima) limeweza tengenezwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Stanford cha jijini Calfornia nchini Marekani . Mabetri ya Lithium-ion ndiyo yanayotumika zaidi katika vifaa vingi vya elektroniki, ila makosa madogo katika utengenezaji wake yanaweza sababisha matatizo ya milipuko.
Milipuko ya simu za Samsung Galaxy Note 7 ulisababisha simu hizo kuondolewa sokoni, hadi sasa chunguzi mbalimbali zinaonesha ilikuwa inasababisha na kosa katika utengenezaji wa betri.
Ingawa katika miaka mingi ya karibuni vifaa vya elektroniki vimeweza endelea sana kiteknolojia ni eneo moja tuu limekuwa na ukuaji mdogo sana wa kiteknolojia – nalo ni betri. Hili limeathiri pia ukuaji wa teknolojia katika vifaa vingine.
Kwa sasa teknolojia hii kutoka chuo cha Stanford inaendelea kuboreshwa na kama itapata mafanikio katika majaribio zaidi kuna uwezekano mkubwa ikatumiwa muda si mrefu.

Monday, January 9, 2017

Thursday, January 5, 2017