Virusi vya ugonjwa
wa ukimwi vinaendelea kujenga kinga dhidi ya dawa za ugonjwa huo
zinazotumika kukinga na kukabiliana na ugonjwa huo,utafiti umesema.
Virusi vya HIV vimeanza kuwa na kinga dhidi ya dawa ya Tenovir katika
asilimia 60 ya visa vyote miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika
kulingana na utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 1998 na 2015.Friday, January 29, 2016
Friday, January 15, 2016
Tuesday, January 12, 2016
6:02 AM
MZM
Simba wa milimani
aliyeuawa katika jimbo la Idaho, nchini Marekani ameshangaza wengi
kutokana na hali kwamba alikuwa na meno ya ziada kichwani.
Meno hayo kamili yanachomoza kutoka kwenye paji la uso na kuonekana kama pembe.Simba huyo aliuawa na wawindaji walioidhinishwa tarehe 30 Desemba.
Idara ya Wanyamapori na Samaki ya Idaho imesema meno hayo huenda ni masalio ya pacha ambaye labda alifariki akiwa tumboni, au labda inatokana na saratani.
12:37 AM
MZM
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.
Messi
mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku
Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata
7.86%.Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita.
Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.
12:34 AM
MZM
Wachezaji wa Arsenal
Droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la Fa imetoka huku timu za ligi kuu ya England zikipangwa na zile za daraja la chini.
Arsenal,
ambao ni mabingwa watetezi wao wamepangwa kukipiga na timu ya Burnley,
Huku Chelsea wao wataanzia ugenini kwa kucheza na Mshindi wa mchezo kati
ya Northampton Town au Mk Dons.Man City wao watakipiga na mshindi wa mchezo wa Wycombe Wanderers au Aston Villa. Huku majirani zao Man United wao watakipiga na Derby County.
West Ham, wanasubiri mshindi wa mchezo unaowakutanisha Exeter City dhidi ya majogoo wa Anfield Liverpool.
Michezo hii ya raundi ya nne itachezwa January 29 mpaka Februari 1.
Subscribe to:
Posts (Atom)