Germanwings: Madaktari watoe siri za marubani
Wachunguzi kutoka Ufaransa, wamependekeza sheria kali inayozuia madaktari kufichua siri za marubani wagonjwa iondolewe.
Wanasema iwapo sheria hiyo isingelikuwepo , ajali iliyosababishwa na rubani mwenza aliyekuwa amezongwa na mawazo isingelitokea.Wachunguzi hao pia wanasema haifai kuwa marubani wanaruhusiwa wenyewe kujitathmini hali yao ya kiafya.
Wanatarajiwa kutoa baadhi ya mapendekezo waliyopata kutoka kwa data ya kifaa cha kurekodi sauti ya ndege hiyo.
Ripoti hiyo ni pamoja na hali ya kiakili ya rubani huyo na usalama wa chumba cha rubani pamoja na hali ya kiafya ya marubani.
Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps.
Ilifahamika baadaye kuwa Lubitz alikuwa na msongo wa mawazo, baada ya kukosana na mpenziwe wa kike, lakini sheria za kisiri za Ujerumani zinazuia madaktari kutoa siri za ugonjwa wa wateja kwa waajiri.
0 comments:
Post a Comment