Thursday, April 28, 2016


Madhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam
Leo imekuwa siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Kisa na maana,,,,mafuriko.
Wenyeji walitatazikika kuendesha shughuli zao za kawaida
 Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki.
Maji kila mahali 
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo muundo msingi wa barabara za miji ya Nairobi na Dar es Salaam haziwezi kumudu.
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.

 Magari mengi yamekwama barabarani 
Wenyeji sasa wameanza kuhoji uwezo wa muundo msingi wa maji taka wa mji huo wa Dar es Salaam hususan ukizingatia kuwa ndio sasa msimu wa mvua umeanza.
Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara ya Dar es Salaam.

 Wenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani 
Nchini Kenya hali sio tofauti.
Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa.
 

Thursday, April 21, 2016

 
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekiri Serikali kupoteza mapato mengi ya ndani kwa miaka ya nyuma kutokana na mapungufu ya Sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 1997 na Sheria ya Usimamizi wa kodi. Mapungufu ya Sheria hizo yaliikosesha nchi mapato kwa kile kilichodaiwa kuwepo kwa misululu mingi ya misamaha ya kodi, iliyotolewa kwa sababu mbalimbali.
Katika mafunzo maalumu ya elimu kwa mlipa kodi yaliyotolewa kwa wamiliki wa mabasi nchini TABOA na mamlaka hiyo yalikusudia kutoa uelewa na umuhimu wa kutumia mashine za kutolea risiti pamoja na sheria mpya za kodi kama zilizofanyiwa marekebisho.

BAADA ya jana kutolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Al Ahly ya Misri, Yanga sasa imepangiwa kucheza na Sagrada Esperance ya Angola kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Sagrada wako nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ya Angola wakiwa na alama 9 pekee.

Yanga sasa itaanzia nyumbani Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kati ya Mei 6 na 8 kabla ya kurudiana kati ya Mei 17-18.

Mechi nyingine zitakuwa kama ifuatavyo:

MO Bejaja(Algeria) vs Esparance (Tunisia)

Stade Malien(Mali)vs FUS Rabat( Morocco)

Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana(Gabon)

http://www.channelten.co.tz/wp-content/uploads/2016/01/tbs-may16-2013113.jpg

Wizara ya Viwanda na Biashara imeliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kusimamia na kuhakikisha wazalishaji wa bidhaa nchini wanakuwa na alama ya Msimbomilia au BarCode inayotambulisha bidhaa husika lengo likiwa ni kuondokana na bidhaa feki.
Wizara hiyo imesema kuwepo kwa alama hiyo kutaziwezesha bidhaa za nchini kuwa na soko na hatimaye kuepukana na bidhaa toka nje ya nchi ambazo viwango vyake vya ubora vinatiliwa shaka.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Odilo Majengo amesema Wizara yake ipo katika kuvifanyia maboresho viwanda vya ndani ili vizalishe bidhaa zenye ubora na zenye kutambulika nje ya nchi hivyo matumizi ya BarCode yatasaidia kuinua viwango vya ubora wa bidhaa nchini.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Kampuni inayotoa nembo hizo za BarCode ya GSI wamesaini hati ya makubaliano ya kuhakikisha wafanyabiashara wa ndani wanatambulika kwa kutumia nembo hiyo ya biashara.

Wednesday, April 20, 2016


Kaimu kamishina wa madini, Ally Samaje
MADINI aina ya Tanzanite ya thamani ya Sh bilioni 2.5 yaliyokamatwa mwaka jana yakitoroshwa nje ya nchi, yatauzwa kwa mnada wa hadhara wakati wa maonesho ya kimataifa ya madini ya vito yaliyoanza jana hapa.
Madini hayo yalikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) yakitaka kutoroshwa kwenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kisheria na baada ya kukamatwa yametaifishwa na serikali.
Akizungumza jana jijini hapa wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ya tano ya madini ya vito ya siku tatu, Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Ally Samaje, alisema madini hayo yatapigwa mnada katika maonesho hayo ikiwa ni sehemu ya kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.

Thursday, April 14, 2016



RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein jana Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa.

Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7.Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Sunday, April 3, 2016


Wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza wanatumia madawa yaliyopigwa marufuku
Serikali ya Uingereza imeanzisha uchunguzi wa dharura kufuatia ufichuzi kuwa wachezaji nyota wa kandanda nchini Uingereza wamekuwa wakitumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.
Gazeti la Sunday Times limechapisha rhttps://www.blogger.com/blogger.g?blogID=5420544876886876991#editor/target=post;postID=5548928251777649508ipoti ya uchunguzi iliyothibitisha kuwa sio tu wasakataji dimba bali hata waendesha baiskeli, wachezaji Kriketi na hata wachezaji wa tenisi wamekuwa wakipokea matibabu kutoka kwa daktari mmoja ambaye anajulikana kwa kupeana madawa hayo yaliyopigwa marufuku ya kututumua misuli.
Daktari Mark Bonar ambaye anazahanati yake mjini London Uingereza amekuwa akiwatoza wachezaji nyota maelfu ya pauni za Uingereza kwa matibabu hayo fiche ambayo imegunduliwa kuwa ni matibabu ya madawa yaliyopigwa marufuku na shirikisho la kupambana na madawa haramu WADA.