Thursday, April 21, 2016

http://www.channelten.co.tz/wp-content/uploads/2016/01/tbs-may16-2013113.jpg

Wizara ya Viwanda na Biashara imeliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kusimamia na kuhakikisha wazalishaji wa bidhaa nchini wanakuwa na alama ya Msimbomilia au BarCode inayotambulisha bidhaa husika lengo likiwa ni kuondokana na bidhaa feki.
Wizara hiyo imesema kuwepo kwa alama hiyo kutaziwezesha bidhaa za nchini kuwa na soko na hatimaye kuepukana na bidhaa toka nje ya nchi ambazo viwango vyake vya ubora vinatiliwa shaka.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Odilo Majengo amesema Wizara yake ipo katika kuvifanyia maboresho viwanda vya ndani ili vizalishe bidhaa zenye ubora na zenye kutambulika nje ya nchi hivyo matumizi ya BarCode yatasaidia kuinua viwango vya ubora wa bidhaa nchini.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Kampuni inayotoa nembo hizo za BarCode ya GSI wamesaini hati ya makubaliano ya kuhakikisha wafanyabiashara wa ndani wanatambulika kwa kutumia nembo hiyo ya biashara.

“Bar Code ni nembo ya kibiashara inayotambulisha bidhaa mbalimbali Duniani ambapo kwa Tanzania, nembo hiyo imeanza kutumika na baadhi ya wafanyabiashara ili kuondokana na bidhaa feki”. alisema Fatmah Kange Mkurugenzi Mkuu wa GSI Tanzania.

0 comments: