
Moto 
 mkubwa wa gesi umelipuka na kuteketeza nyumba eneo la Hospitali ya 
Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam jana jioni  kutokana na Bomba la 
gesi kutoka Songo Songo, Lindi/Mtwara kwenda Ubungo, Dar, kupasuka na 
kusababisha moto mkubwa uliozua taharuki kwa wakazi na wafanyabiashara 
wanaozunguka eneo la Buguruni Mnyamani.
Taarifa
 za awali za zilisema bomba hilo lililipuka baada ya mafundi wa Dawasco 
waliokuwa wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao ya maji, 
kulitoboa bomba hilo la gesi kimakosa.
Akithibitisha
 kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar 
es salaam, Benedict Kitalika, amesema  kwamba mafundi hao walikuwa 
wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao, na ndipo wakatoboa bomba 
hilo kimakosa.
Kamanda Kitalika ameendelea kwa kusema kwamba wameshawasiliana na watu wa Mtwara na kufunga bomba hilo, ili kupunguza kasi ya gesi.
Kamanda Kitalika ameendelea kwa kusema kwamba wameshawasiliana na watu wa Mtwara na kufunga bomba hilo, ili kupunguza kasi ya gesi.
Madhara
 yaliyosabaishwa na moto huo ni kuteketea kwa baadhi ya vibanda vya 
wafanyabiashara, kuungua kwa nguzo za Tanesco na nyumba moja imeteketea 
kabisa lakini hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki dunia wala kujeruhiwa 
kutokana na moto huo.
 RSS Feed
 Twitter

1:26 AM
MZM
 Posted in 
0 comments:
Post a Comment