Showing posts with label Tz. Show all posts
Showing posts with label Tz. Show all posts

Wednesday, January 10, 2018


Moto  mkubwa wa gesi umelipuka na kuteketeza nyumba eneo la Hospitali ya Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam jana jioni  kutokana na Bomba la gesi kutoka Songo Songo, Lindi/Mtwara kwenda Ubungo, Dar, kupasuka na kusababisha moto mkubwa uliozua taharuki kwa wakazi na wafanyabiashara wanaozunguka eneo la Buguruni Mnyamani.

Friday, July 22, 2016

Tume ya vyuo vikuu nchini TCU, imevizuia vyuo sita nchini kufanya udahili wa wanafunzi kwenye msimu wa masomo wa 2016/17.
WAZIRI-WA-ELIMU
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako (Kulia)

Hatua hiyo imechukuliwa na tume hiyo kutokana na vyuo hivyo kutokidhi viwango vya elimu vilivyokuwa vikiitoa.
Vyuo hivyo ni pamoja na:
1. International Medical and Technological University (IMTU) – all programmes.
2. St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS) – all programmes.
3. University of Bagamoyo (UoB) – all programmes.
4. St. Joseph University College of Engineering (SJUCET) – all programmes.
5. University of Dodoma (UDOM) – Doctor of Medicine Programme
6. State University of Zanzibar (SUZA). – Doctor of Medicine Programme.

Wednesday, June 8, 2016


Nchini kenya waziri wa fedha Henry Rotich leo amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya matumizi ya pesa za serikali katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Bajeti hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo. Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.
Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.
Kama ilivyo ada bajeti inaposomwa kuna wale wa wanaofaidi na wale wanaopoteza. Gesi ya kupikia na chakula cha mifugo umeondolewa ushuru, Huku ushuru wa petroli na mafuta taa ukiongezwa. Bidhaa za mafuta ya urembo zikiwekewa ushuru wa asilimia kumi kwa mara ya kwanza.
Waziri ametenga shilingi bilioni 4.3 kwa huduma za bure za wanawake wajawazito kujifungua,milioni 19.7 kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 na shilingi milioni 7.9 kwa watoto mayatima.


Nchini Tanzania makadirio ya bajeti ya mwaka 2016 na 2017 ni trilioni 29,5 pesa za Tanzania ikiizidi bajeti ya mwaka wa 2015 na 2016 kwa trilioni 7.1.
Waziri wa Fedha nchini Tanzania Phillip Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 18.46 zitatokana na jumla ya mapato ya ndani.
Kiwango hicho kimezidi shilingi trilioni 3.64 za bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya shilingi trilioni 4.82.
Shilingi trilioni 17.72 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zikitengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Bwana Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.88 zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.
Makadirio ya bajeti nchini Uganda mwaka 2016 na 2017 iliyosomwa leo ni ya jumla ya dola bilion 7.5 ambayo ni sawa na trillioni 27. 3 pesa za Uganda, tofauti na bajeti ya mwaka uliopita ya mwaka 2015 na 2016 ambayo ilikuwa ni dola bilioni 6.9.
Bajei kubwa mwaka huu nchini Uganda imeelekezwa kwa wizara ya kazi na uchukuzi ambayo ilipewa dola blioni 1.1 huku wizara ya ulinzia ikipewa dola milioni 435. Wizara ya afya imepata dola milioni 525.
Wizara ya nishati na maendeleo ya madini ilipata dola milioni 695 huku Wizara ya kilimo ambayo nidiyo muhimu nchi Uganda ikiewa dola milioni 522.

Monday, May 30, 2016

 
Chuo kikuu cha Dodoma
Wanafunzi katika chuo kikuu cha Dodoma nchini Tanzania wamefukuzwa chuoni humo baada ya kuzuka kwa mgogoro kati ya serikali na wahadhiri wa chuo hicho.
Wanafunzi hao waliagizwa kuondoka katika chuo hicho kufikia saa kumi na mbili jioni siku ya Jumapili.

Ilani
Ilani hiyo imesema kuwa kulikuwa na makosa katika mafunzo ya wanafunzi wanaosomea shahada ya elimu ikiwemo sayansi,hesabati,teknolojia hivyobasi serikali imewataka wanafaunzi hao kuondoka chuoni humo hadi ilani nyengine itakapotolewa.
Maelezo kuhusu mgogoro huo kati ya wahadhiri wa chuo hicho na serikali hayajulikani.

Saturday, May 21, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

Friday, May 20, 2016

Swala
Shambulio lilitekelezwa wakati wa swala jioni
Polisi nchini Tanzania wanawazuilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika shambulio katika msikiti mmoja mjini Mwanza magharibi mwa nchi hiyo.
Watu watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi jijini humo, Ahmed Msangi, uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia mapanga na kuongeza kuwa, polisi wanachunguza chanzo cha shambulizi hilo.
Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, wamesema shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wasiopungua 15.