MWANAMKE
mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same
mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa
kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani
ya shilingi bilioni 2.5.
Madawa
hayo yalikutwa kwenye nyumba moja iliyopo eneo la
Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Ununio, Tegeta jijini Dar es Salaam, ambayo ni mali ya Mbunge wa CCM (Jina linahifadhiwa) wa jimbo moja la mikoa ya Kanda ya Ziwa, Uwazi limefukunyua.
Taarifa
toka vyanzo mbalimbali makini, zinasema majirani wa nyumba hiyo walikuwa
na mashaka na kinachofanyika ndani ya nyumba hiyo, kwani licha ya
ukubwa na kukamilika kwa ujenzi wake, lakini haikuwa ikikaliwa na mtu na
mara chache, watu walionekana wakiingia na kutoka bila kujulikana
walichokuwa wakikifanya.
Kutokana
na hali hiyo ya wasiwasi, wasamaria wema walitoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi ambalo liliifanyia kazi habari hiyo na kufika kwenye nyumba hiyo
na kujaribu kugonga lakini bila mafanikio yoyote.
“Baada ya
kugonga, ndipo polisi hao walipoamua kuvunja mlango na kufanya upekuzi
katika sehemu zote ndani ya nyumba hiyo, ambapo walifanikiwa kulikuta
sanduku ambalo baada ya kufunguliwa, zikagundulika kilo 35 za madawa ya
kulevya aina ya Heroin,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia zoezi
hilo.
Kamanda
wa Kikosi Cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP
Godfrey Nzowa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
baada ya kukamata shehena hiyo, vijana wake walijikuta katika wakati
mgumu wa kumjua mmiliki wa nyumba hiyo.
Baada ya
kutafuta nyaraka mbalimbali, hatimaye waligundua kuwa nyumba hiyo
inamilikiwa na mbunge huyo wa zamani ambaye alitafutwa na kuhojiwa kwa
saa kadhaa, ambapo alikiri kuimiliki, lakini akidai kwa muda huo,
alikuwa ameipangisha kwa watu aliowataja, bila kujua shughuli iliyokuwa
ikifanyika ndani yake.
Inadaiwa
kuwa baada ya kupata ushirikiano huo kutoka kwa mbunge huyo, askari
waliingia mtaani kuwasaka wapangaji hao, ambapo Septemba 15, mwaka jana,
saa saba mchana, walifanikiwa kumkamata Doreen, akiwa shambani kwake,
eneo la Ruaha Mbuyuni mkoani Iringa alikokuwa akivuna vitunguu, bamia na
bilinganya.
“Tulifanya
uchunguzi na tayari watu watano wameshakamatwa akiwemo Doreen, nyumba
hiyo waliifanya kama ghala la kuhifadhia madawa na mtu mmoja bado
tunaendelea kumsaka, baadhi ya waliokamatwa tulikuwa tukiwasaka kwa muda
mrefu,” alisema Kamanda Nzowa.
Aliwashukuru
wananchi kwa ushirikiano wao na kuwaomba waendelee hivyo na kwamba
donge nono litatolewa kwa watakaofanya hivyo huku majina yao
yakihifadhiwa.Gazeti hili lilimfikia Mbunge huyo mmiliki wa nyumba kwa
njia ya simu, lakini alikataa kulizungumzia suala hilo, akidai liko
chini ya polisi.
“Naomba
suala hili umuulize Kamanda Nzowa, mimi siwezi kulizungumzia kwa vile
lipo chini ya uchunguzi wao, pamoja na kwamba nawatambua hao wapangaji
lakini siwezi kusema lolote,” alisema.
0 comments:
Post a Comment