Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Umoja
usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa
jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye
umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa
urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na
sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya
kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa
mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho
mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.