Junaid Hussain
Marekani imesema mpiganaji wa Kiingereza, ambaye alijiunga na kundi la Islamic State ameuawa katika shambulio la anga nchini Syria.
Junaid Hussain ambaye alikuwa akiendesha kampeni za kundi hilo la Islamic State kupitia mitandao ya kijamii na kufanya kazi kubwa kuwavuta na kuwaingiza katika kundi hilo, raia wa kigeni.
Mwenyekiti wa kamati inayohusika na masuala ya ulinzi wa nyumbani nchini Marekani Michael Mc Caul amesema kijana huyo alikuwa akiongoza harakati za kundi hilo lenye itikadi kali kwa njia ya mtandao.
Hata hivyo mke wa Junaid Hussain amekanusha ripoti kwamba mume wake ameuawa katika mashambulizi hayo ya anga yaliyofanywa karibu na mji wa Ragga.
0 comments:
Post a Comment