Shirika la Umoja
wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF, limesema kuwa
makundi yaliyojihami nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, yamewaachilia
watoto mia moja sitini na watatu.
Watoto hao waliachiliwa mjini
Batangafo, baada ya majadiliano kati ya shirika hilo na makundi hayo ya
waasi mwezi Mei mwaka huu, kama sehemu ya mpango wa amani.Tangu makubaliano hayo jumla ya watoto mia sita na hamsini wameachiliwa na makundi hayo.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kati ya watoto elfu sita na kumi wanazuiliwa na makundi hayo ya waasi, wengi wao wakitumika kama wanajeshi, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza nchini humo mwaka wa 2013.
0 comments:
Post a Comment