Mchoraji wa miundo ya magari nchini 
India Sudhakr Yadav amejaribu kuweka rekodi ya pili ya Guiness kwa 
kutengeneza gari analotumai litakuwa ndilo kubwa zaidi duniani.
Gari
 hilo, ambalo limeundwa likifanana na gari aina ya Ford Toure 
lililoundwa mwaka 1922, lina urefu wa futi 26 (mita 8) kwenda juu na 
ukubwa wa futi 50 lina ukubwa maradufu wa basi lililo na ghorofa mbili 
mjini London.Bwana Yadav tayari anashikilia rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuwa na baiskeli ndefu zaidi duniani.
Mchoraji huyo wa miundo ya magari anamiliki makavazi ya magari katika mji wa Hyderabad ulioko kusini mwa India ambapo anaonyesha mitindo tofauti ya magari.
Magari hayo yana maumbo na ukubwa tofauti .
''Tunalenga kuvunja rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuunda gari kubwa duniani. Ni rekodi mpya na nina matumaini nitaipata," alisema.
Anatarajia gari hilo liwe na mngurumo sawa na wa magari ya mbio za langalanga au Formula One.
Baiskeli yake ya magurudumu matatu ni ndefu zaidi ya gari hilo ikiwa na futi 41.5 kwenda juu.
 RSS Feed
 Twitter

10:47 AM
MZM
 Posted in 
0 comments:
Post a Comment