Thursday, October 8, 2015

http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/10/08/151008115839_bard_prison_initiative_512x288_bardprisoninitiative.jpg

Kundi la wafungwa kutoka New York limeshinda mdahalo dhidi ya kundi kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, chuo kilichoorodheshwa bora zaidi duniani.
Wafungwa hao kutoka Eastern New York Correctional Facility walikuwa wamewaalika wanafunzi hao kutoka Harvard kwa shindano la mjadala gerezani.
Kwenye mdahalo huo, wafungwa walitetea msimamo kwamba watoto wa wazazi walioingia Marekani kinyume cha sheria wanafaa kukataliwa shuleni.
Mdahalo huo uliamuliwa na jopo lisiloegemea upande wowote.
Muda mfupi baada ya kushindwa, wanafunzi hao wa Harvard walijitetea kwenye ukurasa wa timu yao kwenye Facebook.
Gereza hilo hutoa kozi za mafunzo kwa wafungwa kupitia ushirikiano na chuo cha Bard kilichoko karibu.
Hii si mara ya kwanza kwa wafungwa hao kushinda wasomi.
Miaka miwili tangu kuanzishwa kwa klabu yao ya midahalo, wamekabiliana na kushinda timu kutoka Chuo Kikuu cha Vermont na Chuo cha Jeshi la Marekani cha West Point.
Ushindi huo wao dhidi ya wasomi hao wa Harvard hata hivyo ndio mkubwa zaidi kwani timu hiyo ya Harvard ndio mabingwa wa kitaifa na dunia.

0 comments: