Rapper Chidi Benz amefanikiwa kuirudisha afya yake baada ya kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Mapema mwaka huu katika kituo
kimoja cha runinga Chidi Benz alikiri kutumia Madawa ya kulevya na
kuomba msaada ambapo meneja Diamond na Tip Top Connection, Babu Tale
akishirikiana na Kalapina walimsaidia na kumpeleka katika kituo cha
Bagamoyo Sober House ambacho kilimsaidia kuachana na Matumizi ya madawa
ya kulevya.
Jumatano hii katika mitandao ya
kijamii kumesambaa picha mpya za rapper huyo zikimuonyesha jinsi
alivyopendeza hali ambayo imewafanya mashabiki kumpongeza Tabu Tale.
Chid Benzi akiwa na Babu Tale
0 comments:
Post a Comment