Kama
tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi
wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu
kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa
wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.
Tuesday, December 27, 2016
Sunday, November 27, 2016
Thursday, November 10, 2016
Sunday, October 30, 2016
12:17 PM
Unknown
Mapema Jumamosi hii zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii:
Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa kueneza habari hiyo ni batiliWasanii wakimataifa ambao tayari uwepo wao umetangazwa ni pamoja na Yemi Alade wa Nigeria, Jose Chameleone wa Uganda pamoja na Tekno wa Nigeria.
Hii ni list ya wasanii wa Tanzania.
1. Ben Pol
2. Nandy
3. Christian Bella
4. Fid-Q
5. Weusi
6. Roma
7. Chegge
8. Dogo Janja
9. Billnass
10. Stamina
11. Jux
12. Barnaba
13. Maua Sama
14. Darassa
15. Vanessa Mdee
16. Sholo Mwamba
17. Jay Moe
18. Msami
19. Juma Nature
20. Snura
21. Baraka Da Prince
22. Shilole
23. Manfongo
24. Belle 9
25. Lord Eyes
26. Young Dee
27. Raymond
28. Mr. Blue
29. Alikiba
Source
Thursday, October 27, 2016
Sunday, July 31, 2016
Friday, July 22, 2016
6:15 AM
MZM
Tume ya vyuo vikuu nchini TCU, imevizuia vyuo sita nchini kufanya udahili wa wanafunzi kwenye msimu wa masomo wa 2016/17.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako (Kulia)
Hatua hiyo imechukuliwa na tume hiyo kutokana na vyuo hivyo kutokidhi viwango vya elimu vilivyokuwa vikiitoa.
Vyuo hivyo ni pamoja na:
1. International Medical and Technological University (IMTU) – all programmes.
2. St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS) – all programmes.
3. University of Bagamoyo (UoB) – all programmes.
4. St. Joseph University College of Engineering (SJUCET) – all programmes.
5. University of Dodoma (UDOM) – Doctor of Medicine Programme
6. State University of Zanzibar (SUZA). – Doctor of Medicine Programme.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako (Kulia)
Hatua hiyo imechukuliwa na tume hiyo kutokana na vyuo hivyo kutokidhi viwango vya elimu vilivyokuwa vikiitoa.
Vyuo hivyo ni pamoja na:
1. International Medical and Technological University (IMTU) – all programmes.
2. St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS) – all programmes.
3. University of Bagamoyo (UoB) – all programmes.
4. St. Joseph University College of Engineering (SJUCET) – all programmes.
5. University of Dodoma (UDOM) – Doctor of Medicine Programme
6. State University of Zanzibar (SUZA). – Doctor of Medicine Programme.
5:58 AM
MZM
Mchekeshaji Ismail Issa Makombe ‘Kundambanda’ amefariki dunia usiku
wa kuamkia Ijumaa hii baada ya kusumbuliwa na matatizo ya tumbo kwa muda
mrefu.

Mwigizaji huyo ambaye pia aligombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwao Mtwara.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Mwenyekiti wa Chama cha wasanii wa Vichekesho Tanzania, Mkono Wa Mkonole amethitisha kutokea kwa msiba huo.
“Kweli ndugu yetu ametutoka na kwa taarifa zisizo rasmi kesho wanazika, lakini sisi kama wasanii wa vichekesho leo jioni tunakutana na kupanga jinsi ya kuweza kuhudhuria mazishi ya ndugu yetu,” alisema Mkonole.
Mwigizaji huyo ambaye pia aligombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwao Mtwara.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Mwenyekiti wa Chama cha wasanii wa Vichekesho Tanzania, Mkono Wa Mkonole amethitisha kutokea kwa msiba huo.
“Kweli ndugu yetu ametutoka na kwa taarifa zisizo rasmi kesho wanazika, lakini sisi kama wasanii wa vichekesho leo jioni tunakutana na kupanga jinsi ya kuweza kuhudhuria mazishi ya ndugu yetu,” alisema Mkonole.
Friday, July 15, 2016
Saturday, July 2, 2016
9:05 AM
MZM
Mkhitaryan
Mshambuliaji wa klabu ya Borussia
Dortmund Henrikh Mkhitaryan amesajiliwa na klabu ya Manchester United
,kulingana na klabu hiyo ya Ujerumani.
Afisa mkuu wa Dortmund
Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa
United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa
msimu ujao.''Iwapo tungekataa mchezaji huyo angekuwa huru mwaka 2017'' ,Watzke aliambia mtandao wa Dortmund.
United tayari imewasajili wachezaji wawili msimu huu akiwemo beki Eric Baily na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.
Sunday, June 26, 2016
4:48 AM
MZM

Historia ya Mnara ule ilianza mwaka 1889, kisha, kabla na
baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) hadi Vita Kuu ya Pili
ya Dunia (1939 - 1945).
Kwa ufupi Sanamu ya mwanzo kukaa pale ni sanamu ya Herman Von Wissman, Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir Ibn Salim Al Harthi, mtawala/sultani
wa Pangani Tanga.
Kwa ufupi Sanamu ya mwanzo kukaa pale ni sanamu ya Herman Von Wissman, Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir Ibn Salim Al Harthi, mtawala/sultani
wa Pangani Tanga.
2:36 AM
MZM
June 24 2016 Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa ‘TAMISEMI’ imetangaza majina ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka
2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za
Serikali, Kwa urahisi zaidi unaweza kuyaona majina yote kwenye hii link hapa
Friday, June 17, 2016
3:13 PM
MZM

Rapper Chidi Benz amefanikiwa kuirudisha afya yake baada ya kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Mapema mwaka huu katika kituo
kimoja cha runinga Chidi Benz alikiri kutumia Madawa ya kulevya na
kuomba msaada ambapo meneja Diamond na Tip Top Connection, Babu Tale
akishirikiana na Kalapina walimsaidia na kumpeleka katika kituo cha
Bagamoyo Sober House ambacho kilimsaidia kuachana na Matumizi ya madawa
ya kulevya.
Wednesday, June 8, 2016
2:54 PM
MZM
Nchini kenya waziri wa fedha Henry
Rotich leo amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya matumizi ya pesa
za serikali katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Bajeti hiyo ya
jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia
ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo.
Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza
deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.
Kama ilivyo ada bajeti inaposomwa kuna wale wa wanaofaidi na wale wanaopoteza. Gesi ya kupikia na chakula cha mifugo umeondolewa ushuru, Huku ushuru wa petroli na mafuta taa ukiongezwa. Bidhaa za mafuta ya urembo zikiwekewa ushuru wa asilimia kumi kwa mara ya kwanza.
Waziri ametenga shilingi bilioni 4.3 kwa huduma za bure za wanawake wajawazito kujifungua,milioni 19.7 kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 na shilingi milioni 7.9 kwa watoto mayatima.
Nchini Tanzania makadirio ya bajeti ya mwaka 2016 na 2017 ni trilioni 29,5 pesa za Tanzania ikiizidi bajeti ya mwaka wa 2015 na 2016 kwa trilioni 7.1.
Waziri wa Fedha nchini Tanzania Phillip Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 18.46 zitatokana na jumla ya mapato ya ndani.
Kiwango hicho kimezidi shilingi trilioni 3.64 za bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya shilingi trilioni 4.82.
Shilingi trilioni 17.72 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zikitengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Bwana Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.88 zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.
Makadirio ya bajeti nchini Uganda mwaka 2016 na 2017 iliyosomwa leo ni ya jumla ya dola bilion 7.5 ambayo ni sawa na trillioni 27. 3 pesa za Uganda, tofauti na bajeti ya mwaka uliopita ya mwaka 2015 na 2016 ambayo ilikuwa ni dola bilioni 6.9.
Bajei kubwa mwaka huu nchini Uganda imeelekezwa kwa wizara ya kazi na uchukuzi ambayo ilipewa dola blioni 1.1 huku wizara ya ulinzia ikipewa dola milioni 435. Wizara ya afya imepata dola milioni 525.
Wizara ya nishati na maendeleo ya madini ilipata dola milioni 695 huku Wizara ya kilimo ambayo nidiyo muhimu nchi Uganda ikiewa dola milioni 522.
Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter





