Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Li
Zhenghua 24, amekutwa akifanya jaribio la kumla Mtoto wake aliyejifungua
siku chache zilizopita, baada ya kumkuta taya yake ikiwa imenasa
kuzunguka Mkono wa Mtoto wake.
Tukio hilo la ajabu lilitokea katika Hospitali iliyoko Shenzhen
Kusini mwa jimbo la Guangdong, China ambapo mwanamke huyo alifikishwa
kujifungua na baadaye wahudumu wa Hospitali kufanya jitihada za kutafuta
ndugu zake.
Hata hivyo mwanamke huyo akiwa na siku ya tatu Hospitalini hapo
alikutwa na nesi akiwa katika jaribio la kumng’ata mtoto ambapo
madaktari walitumia nguvu na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye
tayari alikuwa na jeraha mkononi.
0 comments:
Post a Comment