Kwa ufupi
Mzindakaya alisema wagombea wa Chadema Kijiji cha
Lamadi walienguliwa kutokana na kutokidhi vigezo baada ya kuwekewa
pingamizi, huku wakisalia wa CCM pekee.
Mikoani. Mgombea uenyekiti kupitia CCM Mtaa wa
Swea, Kata ya Mkolani, Nyamagana, Mwanza, Pius Mihayo amefariki dunia
ghafla akiwa mtaani kwake, muda mfupi baada ya kupiga kura.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Halifa Hida alisema
mgombea huyo alifariki dunia ghafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na
chanzo cha kifo hicho hakijajulikana... “Sasa kwa mujibu wa taratibu za
uchaguzi, tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa viti
maalumu, nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za
uchaguzi zitakapoandaliwa,” alisema Hida.
Mkoani Arusha msongamano wa kupiga kura, katika
kituo cha Mbauda, Kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo cha mtu
aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.
Tukio hilo lilitokea saa tatu asubuhi katika kituo
hicho ambacho kilikuwa kimefurika watu. Mjomba wa marehemu, Ramadhani
Athumani alisema kifo hicho kimewashtua kwani marehemu hakuwa mgonjwa.
“Marehemu alikuwa ni kinyozi na baada ya kupiga
kura alianguka ghafla,” alisema Athumani na kuongeza kuwa mazishi
yatafanyika leo saa saba.
Wagoma kupitishwa bila kupingwa
Vituko vya uchaguzi vimeendelea katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa ambako pamoja na mambo mengine, baadhi ya wagombea wa CCM
waliopita bila kupingwa wameamua kujitoa baada ya kutishiwa maisha.
Tukio la wagombea kutishiwa maisha lilitokea
wilayani Busega, Mkoa wa Simiyu ambako uchaguzi huo ulikumbwa na vurugu
mbalimbali. Taarifa zilizotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Mzindakaya
zinasema wagombea kupitia CCM katika Mji wa Lamadi, walijiondoa dakika
za mwisho.
Hatua hiyo inadaiwa imetokana na wagombea hao
kutishiwa maisha, kuchomewa moto nyumba zao na kwamba kutoka kwa wafuasi
wa chama kimoja cha siasa.
Mzindakaya alisema wagombea wa Chadema Kijiji cha
Lamadi walienguliwa kutokana na kutokidhi vigezo baada ya kuwekewa
pingamizi, huku wakisalia wa CCM pekee.
“Mpaka sasa saa sita mchana, tumeamua kusitisha
upigaji kura masanduku yote tumeyaondoa, hali si shwari eneo hilo,
askari wamepelekwa kurejesha usalama na kamati ya ulinzi na usalama
wilaya itakaa muda huu kujadili hali hii, ili tukubaliane kama tuendelee
au tusitishe,” alisema Mzindakaya.
0 comments:
Post a Comment