Sunday, April 19, 2015


 wewe  ni  dereva  wa basi la abiria ama  gari  binafsi ?hebu  chukua  hatua ya  kupunguza ajali  leo kwa kujihadhari na  kona  hizi na Iyovi na Kitonga na  kona  nyingine kali kama  hizi nchini kwani maisha  yako ni  dhamani  kubwa na uhai  wake bado tunautamani
 Vema  kuheshimu alama  za barabarani na  kuacha mbwembwe  uwapo  barabarani katika kona kali kama hizi
 Katika kona  kama  hizi  zingatia  alama  za usalama  barabarani  usiwe na haraka  ya  kulipita gari la mbele

Kulipita gari la  mbele katika kona kama  hizi ni kutafuta ajali
Hapa  ni eneo ambalo  watu 19  walipoteza maisha kwa fuso kugongana na basi na Nganga na kisha  kuwaka  moto uzembe  ukiwa ni wa dereva wa basi aliyetaka  kulipita gari la  mbele  katika  kona kali

 
 Usilipite gari katika  kona 
 Alama  zote  za barabarani ni msaada kwa maisha  yako lazima  uziheshimu
 Kona  zote ni hatari kwa usalama  wako hivyo  usihame saiti  yako ili  kukimbia ajali
 Lazima  unapotaka  kulipita gari la  mbele uwe una uwezo wa kuona mbali  zaidi ya mita  100 ama  zaidi
 Dereva makini halipiti gari  la  mbele katika  kona
Kumbuka  ni  heri  kuchelewa  ukafika  salama  kuliko kuendesha kwa haraka na ukafika majeruhi ama maiti tambua Taifa  linakuhitaji familia  inakuhitaji na  wewe  dereva ni msaada wa abiria  wote katika gari lako  na  msaada wa maisha  yako jitambue ,watambue abiria  wako , jilinde utulinde  abiria  wako maisha  yako   ni yetu na uhai  wako ni tegemeo letu epuka ajali zingatia sheria  za barabarani

0 comments: