Wednesday, April 29, 2015




Indonesia imewauwa wasafirishaji nane wa madawa ya kulevya siku ya Jumatano, wakiwemo raia saba wa kigeni, hatua iliyolaaniwa vika nya Australia na Brazil, zilizojaribu kuwaokoa raia wake bila mafanikio.
Indonesia imetete hatua yake hiyo ikiitaja kuwa ni muhimu katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, na kusema haina wasiwasi kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Australia kufuatia mauaji hayo, ilizozitaja kuwa ni hisia za muda ambazo hazitadumu zaidi ya miezi mitatu.
Australia ilimuondoa balozi wake kutoka Indonesia kupinga mauaji hayo yaliyofanyika saa sita za usiku, lakini rais wa Indonesia Joko Widodo amesema alikuwa akitekeleza tu sheria dhidi ya wasafirishaji wa madawa ya kulevya.
Watuhumiwa hao -- wawili kutoka Australia, moja kutoka Brazil na wanne kutoka Nigeria -- waliuawa kwa kupigwa risasi pamoja na Muindonesia moja, licha ya kelele za mataifa ya kigeni na maombi ya huruma kutoka kwa wanafamilia wao.

Wanaharakati wa Indonesia wakiandamana kushinikiza wauza unga wasamehewe.
Mfilipino anusurika dakika za mwisho
Raia wa Ufilipino aliekuwa pia amepangiwa kuuawa alipata msamaha katika dakika za mwisho baada ya mwanamke ambaye alidai kumlaghai na kumbebesha madawa yake kwenda Indonsesia, kujitokeza mbele ya polisi nchini Ufilipino.
Msamaha wa mwanamke huyo Mary Jane Veloso, umesifiwa nchini Ufilipino kama muujiza na zawadi kutoka kwa Mungu, lakini mwanasheria mkuu wa Indonesia Muhammad Prasetyo, alisisitiza kuwa ulikuwa ni uahirishaji tu ili kuruhusu uchunguzi wa polisi.
"Seriakli ya Ufilipino ilituomba tuahirishe kumuuwa Mary Jane, aliombwa kutoa ushahidi ili kufichua kesi za usafirishaji haramu wa binaadamu," alisema Prasetyo na kuongeza kuwa, "hili ndiyo limesababisha kuahirishwa kwa mauaji ya Jane kwa sababu tunaheshimu mchakato wa sheria unaotekelezwa nchini Ufilipino."
Wakili Todung Mulya Lubis akiwa na familia za wa wahanga kabla ya kuuawa kwao.
'Ni hasira za muda tu'
Prasetyo pia alipuuza uamuzi wa Australia kumuondoa balozi wake, akiutaja kama "hisia za muda tu", wakati waziri wa mambo ya kigeni Retno Marsudi alisisitiza nia ya serikali mjini Jakarta kuendeleza mahusiano mazuri na nchi hiyo ambayo ni moja wa washirka wake muhimu zaidi wa kibiashara.
Australia iliendesha kampeni endelevu ya kunusuru raia wake waliokuwa kwenye adhabu ya kifo kwa karibu muongo mmoja, na waziri mkuu Tonny Abbot alisema kitendo cha kuuawa kwao hakikuwa cha huruma na wala hakikuhitajika.
"Tunaheshimu uhuru wa Indonesia lakini tunalaani kilichofanyika na hali haiwezi kuwa tu kama kawaida," Waziri Mkuu Abbott aliwambia waandishi wa habari mjini Canberra. " Nataka kusisitiza kwamba kuna uhusiano muhimu kati ya Australia na Indonesia, lakini uhusiano huu umeathirika kutokana na kilichotokea."
Lakini alitahadharisha dhidi ya kuvuruga biashara na utalii. Waaustralia Andrew Chan na Myuran Sukumaran, viongozi wa genge la usafirishaji wa Heroin linalofahamika kama "Bali Nine" walielezwa na serikali ya Australia kama watu waliyobadilika baada ya kusota miaka kashaa gerezani.
Magari ya wagonjwa yakisafirisha majeneza yaliyobeba miili ya wauza unga baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi.
Nigeria yapigwa na butwa
Nchini Nigeria, mbunge Abike Dabiri-Erewa, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya masuala ya nje ya bunge, ameyaelezea mauaji hayo kuwa ni ya kustusha. Abike amesema aliwatembelea Wanigeria wanne waliouwa katika gereza la Indonesia mwaka 2008, wakati huo kukiwa na Wanigeria 21 waliohukumiwa kifo.
Wakati ikikosoa mauaji hayo, Brazil ambayo inafanya biashara yenye thamani ya dola bilioni tano na taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi katika kanda ya Kusini-Mashariki mwa Asia, itahofia pia kupoteza bishara kubwa ya mauzo ya silaha kwa Indonesia kuhusiana na mgogoro huo.
Mauaji ya Mbrazil Rodrigo Gularte yamekosolewa sana nyumbani, huku familia yake ikidai alikuwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa na hakupaswa kupewa adhabu ya kifo. Gularte alikuwa raia wa pili wa brazil kuuawa nchini Indonesia katika kipindi cha miezi mitatu licha ya maombi binafsi ya huruma kutoka kwa rais Dilma Roussef.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Brazil imesema inatathmini mahusiano yake na Indonesia kabla ya kuamua hatua za kuchukua. Mapema Indonesia ilisema inaangalia upya ununuzi wa awamu ya pili ya ndege za Kibrazil aina ya Ebraer EMB-314 Super Tucano, na mifumo ya makombora iliyokuwa imeagiza, baada ya Brazil kukataa kumruhusu balozi mpya wa Indonesia kushiriki hafla ya utambulisho.
Awali, raia wa Ufaransa aliekuwa miongoni mwa kundi lililouawa alipewa msamaha wa muda baada ya sereikali kuruhusu rufaa yake ya kisheria.

0 comments: