Monday, December 28, 2015

Samia
Makamu wa rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alihudhuria mkutano huo
Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.
Wito wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi umetolewa baada ya kikao cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar katika afisi kuu za chama Kisiwandui.

Saturday, December 12, 2015

Burundi
Watu zaidi ya 200 wameuawa Burundi tangu kuanza kwa machafuko Aprili
Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea.
Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.
Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni.
Miili hiyo imepatikana siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo matatu ya jeshi.
Hannibal
Hannibal amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani Oman tangu 2012
Mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Hannibal, ameachiliwa huru baada ya kutekwa nyara kwa muda na kundi la wapiganaji, duru za kiusalama zinasema.
Kwenye video iliyoonyeshwa kwenye runinga ya Lebanon, mfanyabiashara huyo alionekana akiitisha habari zaidi kuhusu kutoweka kwa mhubiri mashuhuri wa dhehebu la Washia nchini Lebanon Musa al-Sadr. Al-Sadra alitoweka mwaka 1978. Alionekana kwenye video hiyo akiwa amejeruhiwa machoni.
Aliachiliwa huru katika mji wa Baalbek na kupelekwa mjini Beirut, polisi waliambia shirika la habari la AP.
Hannibal, 40, alipatiwa hifadhi na Oman mwaka 2012.

Friday, December 11, 2015

Tanzania
Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.

Tuesday, December 8, 2015

Jackson
Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood
Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti.
Trump, mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump.

Wednesday, December 2, 2015

 
Polisi wenye silaha wakipiga doria katika eneo palipotokea mauaji hayo.
Polisi nchini Marekani imesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa San Bernadino mashariki mwa Los Angeles.
Polisi mjini humo inasema tukio hilo imetokea kwenye kituo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na inawezekana lilihusisha watu watatu wenye silaha ambao wametoroka kwa gari.
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivyalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya silaha ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya pati iliyoandaliwa na Idara ya Afya.