Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood
Nyota wa Hollywood 
Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda 
uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti.
Trump, 
mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha 
Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe 
kuingia Marekani.Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump.
Bw Trump, wakati mmoja amewahi kunukuliwa akikosoa kundi linalotetea haki za watu weusi Marekani la Black Lives Matter.
 RSS Feed
 Twitter

9:17 AM
MZM
 Posted in 
0 comments:
Post a Comment