Wednesday, December 2, 2015

 
Polisi wenye silaha wakipiga doria katika eneo palipotokea mauaji hayo.
Polisi nchini Marekani imesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa San Bernadino mashariki mwa Los Angeles.
Polisi mjini humo inasema tukio hilo imetokea kwenye kituo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na inawezekana lilihusisha watu watatu wenye silaha ambao wametoroka kwa gari.
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivyalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya silaha ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya pati iliyoandaliwa na Idara ya Afya.




Mmoja ya ndugu wa wafiwa akifarijiwa.
Rais wa Marekani Barack Obama amelaani shambulizi hilo na kusema Marekani imekumbwa na tukio la mauaji ya watu wengi ambalo halifanani na jingine lolote duniani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la kijasusi la FBI David Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi haijafahamika.
"Kwa wakati huu ninaelewa moja ya maswahili yenu ni kuhusu tukio hili la kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa hiyo tunaanzia mwanzo kufanya kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili. Tunadhani inaweza kuwa, pia inaweza isiwe lakini tunafanya kazi bega kwa bega nao kuanzia mwanzo. Kama mambo yatabadilika tupo hapa na hakuna hatua yoyote itakayopotea wakati uchunguzi utakapokuwa unaendelea." Alisema

0 comments: