Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja 
kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa 
ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara
 hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa 
ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa 
ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya
 kuathiriwa  na vijidudu vingine.Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye maabara ya aina hii ambayo itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii ina umuhimu kwa kuwa itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na haraka zaidi, hata katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa.
Maabara hiyo inatarajiwa kurahisisha uchunguzi wa magonjwa hatari
Changamoto ambayo ilionekana wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi ni wahudumu kutofika kwa urahisi kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi wa haraka kutokana na umbali na miundo mbinu mibovu.
 RSS Feed
 Twitter

10:46 AM
MZM
 Posted in 
0 comments:
Post a Comment