Mkuu wa shule ya Masimbwe Mwalimu Eliud Sanga
Cheti ambacho ni daraja C ambacho kimetolewa na VETA kwaajiri ya kuruhusu elimu ya ufundi itolewe katika shule hiyo
darasa la ufundi ushonaji
darasa la ufundi magari
darasa la masomo ya kawaida ya sekondari
darasa la komputor
mwalimu mkuu wa shule ya masimbwe Eliud Sanga
Imeelezwa kuwa vijana wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameshindwa
kutumia fulsa ya kielimu kwa kile kinachodaiwa kuwa wilaya ya Ludewa kuwa na shule ya Sekondari
inayotoa elimu ya sekondari na ufundi mbalimbali lakini vijana wengi wa wilaya
hii kushindwa kuitumia shule hii ipasavyo na kuendelea kulalamika kuwa wilaya ya
Ludewa bado haina chuo cha ufundi.
Shule hiyo ambayo inamilikiwa na umoja wa wazazi nchini wa
chama cha mapinduzi inatoa elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi kwa wakati
mmoja ijulikanayo kwa jina la Masimbwe Sekondari imekuwa ikipata ufadhiri
mkubwa kutoka kwa raia wa nchi ya Ujerumani Prof.Ludwige amekuwa akileta zana
mbalimbali za kufundishia masomo ya ufundi karibu kila na kuwalipia ada
wanafunzi waishio katika mazingira magumu imekuwa na wanafunzi wachache tofauti
na matarajio ya uanzishwaji wa shule hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari mapema wiki hii mkuu wa
shule hiyo Mwalimu Eliud Sanga alisema kuwa shule hiyo ni shule pekee katika
mkoa wa Njombe ambayo mwanafunzi anahitimu kidato cha nne na kutoka na vyeti
viwili ambavyo ni cheti cha kidato cha nne na kile cha veta ambapo mwanafunzi
anayehitimu kitado cha nne katika shule hiyo anauwezo wa kuomba ajira katika
ofisi mbalimbali.
Mwalimu Sanga alisema kuwa vijana walio wengi wilayani
hapa wamekuwa mabingwa wa kulalamika na
kusema wilaya ya Ludewa haina chuo cha ufundi hali ambayo sio sahihi kwani
shule hiyo licha ya kutoa elimu ya sekondari pia inatoa mafunzo ya ufundi tu ya
muda mfupi wa miezi mitatu mitatu lakini cha kushangaza wanaosoma shule hiyo ni
wanafunzi wa mikoa ya mbali ndio wanaojua kutumia fulsa.
Alisema mpaka sasa kuna baadhi ya vifaa vulivyoletwa na
mfadhiri Prof.Ludwige havijafunguliwa katika makontena kutokana na uhaba wa
wanafunzi pia kuna baadhi ya wanafunzi waliosoma katika shule hiyo ya Masimbwe
tayari wameshaajiriwa katika ofisi
mbalimbali baada ya kuhitimu kidato cha nne ikiwemo ofisi ya shirika la Tanesco
Ludewa mjini pia mradi wa umeme LUMAMA kata ya mawengi.
“inashangaza kuona vijana wa Ludewa pamoja na wazazi
kushindwa kutumia fulsa hii ambayo iko jirani na badala yake wananufaika vijana
wa mikoa ya mbali kwani mfadhiri wa shule hii analeta vifaa vya ufundi
magari,umeme,ushoonaji, ujenzi na komputor akiwa na lengo la kuwainua vijana wa wilaya ya
Ludewa ili baadae waweze kuajiliwa katika migodi ya chuma na makaa ya mawe lakini
juhudi zake zinaonesha kukatishwa tamaa na wanaludewa wenyewe”,alisema Mwalimu
Sanga.
Mwalimu Sanga alisema kuwa mpaka sasa mfadhiri wa shule hiyo
Prof.Ludwige anawalipia ada wanafunzi wapatao 25 kila mwaka ambao wanatoka katika
mazingira magumu wengi wao wakitokea mikoa ya mbali kutokana na vijana wa
wilaya ya Ludewa kutojitokeza kujiunga na masomo katika shule hiyo.
Alisema kuwa hata baadhi ya viongozi wa Serikali wilayani
hapa hawajui kinachoendelea katika shule ya Sekondari Masimbwe hivyo aliwataka
viongozi hao kuitembelea shule hiyo na kuona masomo yanayotolewa kwani
inawalimu wa kutosha pia inafaulisha vizuri na kuhusu idikadi ya kisiasa
mwalimu Sanga alisema kuwa elimu haina siasa hivyo shule hiyo haibagui
wanafunzi wanaosoma hapo wametoka kadika familia zenye itikadi ya chama gani.
0 comments:
Post a Comment