Mwanamke mmoja
aliyekuwa akitumia choo cha muda, alibebwa na kupelekwa sehemu nyingine
wakati choo hicho kilipoinuliwa juu na tracta kimakosa na kuhamishwa
hadi eneo lingine.
Afisa msimamizi wa eneo hilo la bandari, Rob Parsons alisema mwanamke huyo huenda alidhani alikuwa amepotea alipotoka nje ya choo na kujipata sehemu nyingine ya uwanja.
Bw Parsons "Aliingia chooni na kisha choo hicho kikabebwa na kupelekwa upande mwingine wa bandari yeye akiwa ndani.
"Nafikiri alipatwa na mshangao kiasi au alidhani alikuwa amesafirishwa ghafla hadi upande mwingine wa bandari."
Mark Kempthorne, mkurugenzi wa kampuni ya vyoo ya Andyloos, alisema hiyo si mara ya kwanza kwa dereva wa trekta la kreni kubeba choo kikiwa na mtu ndani, ingawa wakati huu aliyefanya hivyo si wa kampuni yake.
Alisema ni rahisi kufanya kosa kama hilo kwani madereva "hupitia lango la nyuma" wanapoenda kuchukua choo.
Alisema, "Kusema kweli hili wakati mwingine hufanyika. Ni kosa nimelifanya mara kadhaa."
0 comments:
Post a Comment