Tuesday, May 31, 2016
Monday, May 30, 2016
2:02 PM
MZM
Chuo kikuu cha Dodoma
Wanafunzi katika
chuo kikuu cha Dodoma nchini Tanzania wamefukuzwa chuoni humo baada ya
kuzuka kwa mgogoro kati ya serikali na wahadhiri wa chuo hicho.
Wanafunzi hao waliagizwa kuondoka katika chuo hicho kufikia saa kumi na mbili jioni siku ya Jumapili.Ilani hiyo imesema kuwa kulikuwa na makosa katika mafunzo ya wanafunzi wanaosomea shahada ya elimu ikiwemo sayansi,hesabati,teknolojia hivyobasi serikali imewataka wanafaunzi hao kuondoka chuoni humo hadi ilani nyengine itakapotolewa.
Maelezo kuhusu mgogoro huo kati ya wahadhiri wa chuo hicho na serikali hayajulikani.
Thursday, May 26, 2016
1:41 AM
MZM
Mwigizaji Jackline Wolper jana
amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na
kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin
‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.
‘Ni kweli Raj (Harmonize)ni
mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama
mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.
Tuesday, May 24, 2016
Monday, May 23, 2016
9:21 AM
MZM
Kialama cha WhatsApp
WhatsApp
imepitia mabadiliko mengi, na imekuwa kati ya applications zinazotumika
na kupendwa zaidi duniani. Baada ya kununuliwa na Facebook,
waendelezaji walianza kuongeza vitu vipya kama kupiga simu za sauti,
kuweza kutuma mafaili, na kuongezwa kwa usalama zaidi. Kwasasa, WhatsApp
ni moja kati ya application yenye watumiaji wengi zaidi, ikiwa na
angalau watumiaji bilioni moja wanaotumia kikamilifu kila mwezi. Katika
makala hii, tutafahamisha baadhi ya vitu vilivyopo WhatsApp na
havitumiki mara nyingi, na namna vinavyoweza kutumika;
Saturday, May 21, 2016
2:51 AM
MZM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga
kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.
Rais
Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles
Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi akiwa amelewa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Friday, May 20, 2016
12:59 PM
MZM
Polisi nchini
Tanzania wanawazuilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika shambulio
katika msikiti mmoja mjini Mwanza magharibi mwa nchi hiyo.
Watu
watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo
lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku
ya Jumatano.Kwa mujibu wa kamanda wa polisi jijini humo, Ahmed Msangi, uchunguzi wa mwanzo umebaini kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia mapanga na kuongeza kuwa, polisi wanachunguza chanzo cha shambulizi hilo.
Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, wamesema shambulio hilo lilitekelezwa na kundi la watu wasiopungua 15.
12:43 PM
MZM
Staa wa Marekani, Ne-Yo jana usiku alitua jijini Dar es Salaam akitokea Marekani akiwa na ulinzi mkali.
Muimbaji huyo wa ‘Miss Independent’ alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mida ya saa tano kasoro usiku. Staa huyo aliyekuwa amevaa nguo zote nyeusi na kofia ambayo alikuwa ameifunika na hood aliwapungia mkono waandishi wa habari na mashabiki waliokuwa wamejitokeza kumpokea kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye gari na kufunga vioo.
Mlinzi wake pandikizi la mtu, alimzuia staa huyo kutoongea na waandishi wa habari kwa kudai kuwa alihitaji kupumzika kutokana na uchovu wa safari hiyo. Hata hivyo baada ya kuombwa na waandishi wa habari walau wamuulize maswali machache, alifungua kioo cha gari na Ne-Yo kusalimia.
“Fantastic so far,” alijibu Ne-Yo baada ya kuulizwa anajisikiaje kuja Tanzania. “ I am happy to be here looking forward to perform with Diamond and everyone who will be at the show,” aliongeza.
Ne-Yo atatumbuiza Jumamosi hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka linalodhaminiwa na Vodacom. Diamond na wasanii wengine zaidi ya 20 watatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM.

11:38 AM
MZM
Drake amezidi kuonyesha ubora wake kwenye tuzo za BET zitakazofanyika, Juni 26 huko Los Angeles, Marekani.
Mwaka 2016 umekuwa wa neema kwa Drake baada ya kuonekana mara tisa kati ya vipengele sita alivyowekwa akifuatiwa na Beyonce pamoja na Rihanna. Pia albamu yake ya ‘Views’ inazidi kushika namba moja kwenye chati za Billboard baada ya kuuza nakala zaidi ya milioni 1.04 ndani ya wiki mbili tangu alipoiachia mwishoni mwa mwezi Aprili.
Tuzo hizo za BET zitafanyika kwenye ukumbi wa Microsoft Theater, Los Angeles huku Afrika Mashariki tukiwakilishwa na Diamond kwenye kipengele cha Best International Act: Africa lakini pia atafanikiwa kufanya show kwenye tuzo hizo.

Wednesday, May 4, 2016
4:51 AM
MZM
Mvulana wa umri wa miaka 10 nchini Finland ameshangaza wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mvulana
huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua
udhaifu huo uliowezesha mtu kuingia kwenye mtandao huo wa kusambaza
picha na kufuta maoni ya watu.Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kisheria haruhusiwi kutumia mtandao huo hadi atimize umri wa miaka 13.
Facebook, inayomiliki Instagram, ilichukua hatua upesi na kuondoa udhaifu huo.
Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo.
Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.
Wataalamu wa mtandao huo walimfungulia akaunti ndipo aweze kuthibitisha madai yake na akafanikiwa.
- Papa Francis aingia Instagram
- Viongozi maarufu katika Twitter na Instagram
- Mabadiliko katika Instagram yazua hisia kali
Facebook imeambia BBC kwamba imelipa jumla ya $4.3m kwa watu waliogundua udhaifu kwenye mitandao yake.
Malipo hayo hutolewa kama kishawishi kuzuia watu kuuzia wahalifu ugunduzi wao na hivyo kusaidia kampuni husika.
4:37 AM
MZM
Rais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji.
Kanali Bagaza amekuwa akitibiwa kwa muda katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels."Imethibitishwa, rais wa zamani Jean Baptiste Bagaza amefariki dunia akiwa nchini Ubelgiji,2 ameandika mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kwenye Twitter.
"Alikuwa seneta maisha.”
Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu wake Meja Pierre Buyoya Septemba 1987.
Tuesday, May 3, 2016
2:27 PM
MZM
Mamaake aliyekuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap Tupac Shakur ,Afeni Shakur amefariki akiwa na umri wa miaka 69.
Kaunti ya California imethibitisha kifo chake kupitia ujumbe wa Twitter.Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.Alice Faye Williams,alibadilisha jina lake na kuitwa Shakur akiwa mtu mzima alipokuwa mwanaharakati wa kisiasa na kujiunga na vuguvugu la Black Panther.
Alikuwa na mimba ya Tupac mwaka 1971 alipokamatwa na kufungwa jela pamoja na wanachama wengine wa vuguvugu hilo na kukabiliwa na mashtaka ya njama ambayo baadaye yalitupiliwa mbali.
Shakur alikuwa kigezo kizuri cha muziki wa mwanawe na alisimamia muziko wake baada ya kifo chake.
Tupac Shakur alifariki mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25,baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika gari moja.
Mauaji yake bado hayajapata ufafanuzi.
2:22 PM
MZM
Tanzania
inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake
mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .
Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.
Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
- Ivory Coast 8.5%
- Tanzania 6.9%
- Senegal 6.6%
- Kenya 6%
- Zambia 3.4%
- Nigeria 2.3%
- Afrika Kusini 0.6%
Subscribe to:
Posts (Atom)