Friday, May 20, 2016

Staa wa Marekani, Ne-Yo jana usiku alitua jijini Dar es Salaam akitokea Marekani akiwa na ulinzi mkali.
Muimbaji huyo wa ‘Miss Independent’ alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mida ya saa tano kasoro usiku. Staa huyo aliyekuwa amevaa nguo zote nyeusi na kofia ambayo alikuwa ameifunika na hood aliwapungia mkono waandishi wa habari na mashabiki waliokuwa wamejitokeza kumpokea kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye gari na kufunga vioo.
Mlinzi wake pandikizi la mtu, alimzuia staa huyo kutoongea na waandishi wa habari kwa kudai kuwa alihitaji kupumzika kutokana na uchovu wa safari hiyo. Hata hivyo baada ya kuombwa na waandishi wa habari walau wamuulize maswali machache, alifungua kioo cha gari na Ne-Yo kusalimia.
“Fantastic so far,” alijibu Ne-Yo baada ya kuulizwa anajisikiaje kuja Tanzania. “ I am happy to be here looking forward to perform with Diamond and everyone who will be at the show,” aliongeza.
Ne-Yo atatumbuiza Jumamosi hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka linalodhaminiwa na Vodacom. Diamond na wasanii wengine zaidi ya 20 watatumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa linaloandaliwa na kituo cha redio cha Jembe FM.

Baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Ne-Yo alienda kwenye hafla ya Meet and Greet iliyofanyika Club Rouge iliyopo kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
IMG_6599
Warembo waliohudhuria kwenye hafla ya Meet and Greet ya Ne-Yo
Huko akiwa kwenye ulinzi mkali zaidi alisalimiana na wafanyakazi wa Vodacom, CocaCola pamoja na mashabiki waliokuwepo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania aliyekuwepo pia usiku huo alisema kwa mara nyingine tena kampuni hiyo imefanikisha kuletwa kwa msanii mahiri wa kimataifa kuwaburudisha wapenzi wa muziki wa Mwanza.
“Ni kitu kizuri sana kuwa na msanii wa hadhi ya kimataifa kama Ne-Yo hapa Tanzania. Jembeka na Vodacom litakuwa tamasha kubwa, kama hujapata tiketi yako chukua sasa zimebaki chache. Pia balozi wetu Diamond Platnumz atatumbuiza pia Mwanza,” alisema Ferrao.

0 comments: