Mwigizaji Jackline Wolper jana
amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na
kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin
‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.
‘Ni kweli Raj (Harmonize)ni
mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama
mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.
(Picha kwa msaada wa mtandao)
‘’Nisingependa
kumuongelea mwanaume niliyekuwa naye ‘Putin’, nikiona picha
zake,nikisikia jina lake yaani kuna vitu nikiviona kuhusu yeye naumia
sana , na mimi nikimpenda mwanaume nampenda kutoka moyoni, nilijuana
naye mwaka 2012 nilikuwa namzungusha kwasababu watu walikuwa wakiniambia
kabila lao ni waongo, sasa kipindi alivyorudi hapa nchini alinikuta
nipo singo, nilikuwa sipo sawa’’
‘’Katika maisha yangu sijawahi
kumpeleka mwanaume kwa wazazi wangu nilimuamini nikampeleka kwetu na
unajua mwanaume yeyote unayempeleka kwenu hutokubali kuachana naye
kwasababu utakuwa unawaangusha wazazi wako na familia yako na ikiwa
wamempokea vizuri lakini kwanini nimekubali kumuacha’’(analia)
‘’Ni kweli alikuwa mume wa mtu,
baadhi ya watu walikuwa wakiniambia na kunitumia picha siku ambayo
alinivisha pete, n asiku ambayo alinivisha pete nilikuwa sijui ilikuwa
ni sehemu ambayo tulikuwa tunapenda kukaa na kunywa kila siku ananivisha
pete nikakubali baada ya kunivalisha watu wakawa wananiambia kwanini
nimevishwa pete na mume wa mtu sikutaka kumuamini mtu kwa sababu
mahusiano yangu mengi yamekuwa yakiharibika kwa sababu kuwasikiliza
watu, niliziona picha za harusi lakini nilihisi ni harusi tu, sikuelewa
kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi’’
‘’Putin alikuwa akinidanganya
kuhusiana na mke wake na niliamini ndoa nyingi watu wanaoana na kuachana
na aliniambia ni kweli alikua na mwanamke lakini waliachana, lakini
mwanamke aliyekuwa naye ni tofauti na watu walivyokuwa wakiambia yeye
aliniambia kuwa hawajaoana na mwanamke huyo ila walitaka kufunga ndoa,
kiukweli ni mtu ambaye anaweza sana kujielezea alinidanganya sana,
nilimuamini sana kuliko wale watu zaidi ya kumi waliokuwa wakinieleza
ukweli kuhusu yeye sikuwaamini, na wale waliokuwa wananiambia ukweli
hawakuwa wabaya lakini sikuwaelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi
tayari’’ (analia).
‘’Nilitoka naye hapa tukaenda
South Afrika(analia) tulienda kwa ajili ya kusoma nakumbuka ilikuwa
mwezi wa 12 mwaka jana akaniambia ameshalipa kila kitu na ameninulia
gari ya kuendea shule,nikakaa miezi mitatu sikusoma lakini wazazi wangu
walikuwa wanajua nasoma ilikuwa ni lazima nimsitiri mchumba wangu kwa
wazazi wangu nikawadanganya kuwa nasoma, mama yangu alikuwa anampenda
sana mchumba wangu lakini baba yangu hakukubaliana na naye, alikuwa
akisema kuwa kama atanichukua kunipeleka South Afrika basi akamilishe
ishu ya kunivisha pete na kunioa kabisa, akanivisha pete mbele ya wazazi
wangu wakakubaliana baada ya mwezi wangeleta mahali ’’ alisema Jack.
‘’Tulivyofika South Afrika
nilikuwa namfanyia kila kitu kama mke wa mtu, nilikuwa namdanganya mama
nasoma lakini baada ya hapo nikaona mambo hayaendi kwa sababu kuna siku
nilienda salun nikasikia kuwa mke wake naye yupo kule Sauz na alikuwa
ananiaga sana anasafiri anaweza akakaa siku mbili au tatu nikamuuliza
akaniambia sio kweli yupo Kongo’’ alisema Jack.
‘’Siku iliyofuata alikuja
nyumbani akiwa amechelewa, nilikuwa chumbani yeye alikuwa sebuleni
ana’preview’ picha nikataka kumpora simu nikamwambia nimeona picha ukiwa
na mke wako, na mtoto wako, akaniambia alimkuta mwanamke wake kwa kaka
yake akataka kupiga picha naye ndo akapiga, halafu alikuwa anavaa pete
ya ndoa nikamwambia siitaki hiyo pete akaiuza, lakini kuna siku alirudi
akiwa ameivaa ile pete nikakasirika nikamwambia naondoka akanitupia ile
pete kitandani akaniambia nikaitupe chooni’’ alisema Jack.
‘’Kuna kipindi nilikuwa nalewa
sana kutokana na stress, kuna siku nilikuwa ‘location’ nilikuwa nimelewa
hadi nikazima akapigiwa simu akanifuata akanipeleka nyumbani akanivua
nguo zote akaanza kunirekodi na kunipiga picha, lakini nilifanikiwa
kuzifuta, lakini baada ya wiki mbili alinitumia meseji na kunitisha kuwa
kitu atakachonifanya watanzania watafunga macho na sitoamini’’
Alimalizia Jack
Source: Clouds FM
0 comments:
Post a Comment