Kialama cha WhatsApp
WhatsApp
imepitia mabadiliko mengi, na imekuwa kati ya applications zinazotumika
na kupendwa zaidi duniani. Baada ya kununuliwa na Facebook,
waendelezaji walianza kuongeza vitu vipya kama kupiga simu za sauti,
kuweza kutuma mafaili, na kuongezwa kwa usalama zaidi. Kwasasa, WhatsApp
ni moja kati ya application yenye watumiaji wengi zaidi, ikiwa na
angalau watumiaji bilioni moja wanaotumia kikamilifu kila mwezi. Katika
makala hii, tutafahamisha baadhi ya vitu vilivyopo WhatsApp na
havitumiki mara nyingi, na namna vinavyoweza kutumika;
1. Kuweka maandishi yaliyokolea (bold), kiitaliano (italics) na kuyakata maandishi.
Unataka
kutuma ujumbe ambao una muonekano maalumu? Kwa kuweka alama ya nyota
mwanzo na mwisho wa neno, basi utakuwa umelifanya neno kukolea (bold). Kuyalaza maandishi (italics) weka alama ya underscore (_) mwanzo na mwishoni mwa neno, na ukitaka kulikata neno katikati weka alama ya tilde(~) mwanzo na mwisho.
2. Kuzima taarifa za wanaochati kwenye kundi (mute)
Kama
una marafiki wanaopenda kuchati sana na hutaki kuwaudhi kwa kutoka
kwenye kundi, basi unaweza ukazima taarifa kwa saa nane, siku saba au
mwaka mzima. Wewe bonyeza kwenye taarifa za kundi halafu bonyeza mute na
chagua muda unaotaka kutopata taarifa wanapochati. Utakuwa umewaweza
3. Kutuma ujumbe kwa namba nyingi kwa pamoja
Pengine
una taarifa ambayo ungependa kutuma kwa watu wengi kwa pamoja, labda ni
biashara na ungependa kila mtu imfikie inbox kwake. Sini hii inaitwa
Broadcast List na inapatikana juu kabisa upande wa kulia kwenye skrini
yako ya kuchati. Bonyeza Chats -> Broadcast Lists -> New List -> Add contacts, Andika meseji yako na bofya send
4. Kuweka shortcut ya chati yako na mtu kwenye kioo cha simu yako
Labda
una bae na unapenda ukibonyeza mara moja tu kwenye kioo muanze kuchati
bila kuhangaika kuanza kutafuta jina lake lilipo. Fanya hivi, bonyeza
namba yake na kuishikilia kwa muda kwenye chati zenu WhatsApp, kisha
chagua Add Conversation Shortcut. Sini hii inafanya kazi kwenye simu za Android pekee
5. Kujibu ujumbe bila kufungua application yako
Shortcut
hii inapatikana kwenye simu za Android pekee kwa sasa, na inakuwezesha
kujibu meseji ya mtu aliyetuma bila kulazimika kufungua application
yako. Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye Settings -> Notifications -> chagua Always show popup.
6. Zuia mafaili ya Picha, Sauti na Video zisijipakue
Inawezekana
haupendezwi na namna ambavyo Video, sauti na picha hujidownloadi moja
kwa moja na kujaza memori yako. Kama hutaki kujaza memori yako, unaweza
kuzuia kwa kwenda kwenye Settings -> Data Usage -> Media auto-download na utaona sehemu ya kuzima mafaili yasijipakue.
Je ulifahamu mbinu hizi? Tafadhali tujulishe kwa kukomenti kwa akaunti yako ya Google hapa chini
0 comments:
Post a Comment