Mvulana wa umri wa miaka 10 nchini Finland ameshangaza wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mvulana
huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua
udhaifu huo uliowezesha mtu kuingia kwenye mtandao huo wa kusambaza
picha na kufuta maoni ya watu.Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kisheria haruhusiwi kutumia mtandao huo hadi atimize umri wa miaka 13.
Facebook, inayomiliki Instagram, ilichukua hatua upesi na kuondoa udhaifu huo.
Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo.
Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.
Wataalamu wa mtandao huo walimfungulia akaunti ndipo aweze kuthibitisha madai yake na akafanikiwa.
- Papa Francis aingia Instagram
- Viongozi maarufu katika Twitter na Instagram
- Mabadiliko katika Instagram yazua hisia kali
Facebook imeambia BBC kwamba imelipa jumla ya $4.3m kwa watu waliogundua udhaifu kwenye mitandao yake.
Malipo hayo hutolewa kama kishawishi kuzuia watu kuuzia wahalifu ugunduzi wao na hivyo kusaidia kampuni husika.
0 comments:
Post a Comment