James Horner
James
Horner, mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood
ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu
ulimwenguni ya Titanic,amefariki dunia mjini California kutokana na
ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61.
James alipata mafunzo ya
urushaji wa ndege,inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali
hiyo,na ndege binafsi ndogo ambayo alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa
Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii .
Mwandishi huyu na mtunzi wa
tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu
za msanii James Cameron , pamoja na filamu ya A Beautiful Mind,
Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.katika utendaji kazi wake
uliotukuka, James alipewa tuzo ya Oscar kwa filamu ya Titanic na wimbo
uliotawala humo na nyinginezo .
James alipewa tuzo ya ushirika
katika tuzo ya pili kwenye mashairi na msanii Will Jennings kwa wimbo
bora wa asili , na kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika wimbo
maarufu wa My Heart Will Go On, ambao uliimbwa na Celine Dion.
Ajali
hiyo ilitokea katika msitu mzito wa taifa la Marekani wa Los Padres,
Kaskazini mwa Los Angeles, wakati ndege hiyo ikidondoka ilitoa mshindo
mkuu na kuripuka mara tu ilipotua aridhini moto ambao baadaye ulizimwa
na kikosi cha wazima moto wa eneo hilo. Wanaeleza mashuhuda ambao ni
wazima moto.
Msaidizi wa marehemu Horner , Sylvia Patrycja
amethibitisha juu ya kifo hicho kwa kuandika kweny ukurasa wake wa
facebook mwanzoni mwa wiki hii akisema kuwa: "tumempoteza mtu wa kipekee
sana ambaye alikuwa na moyo mkuu wa kujitoa na mtu mwenye kipaji
kisicho elezeka .amekufa wakati anafanya kitu akipendacho. Asante kwa
mchango wako mkubwa na upendo uliokuwa nao tutaonana mbinguni ."