Maofisa
wa afya nchini Sierra Leone wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili wapya
wanaougua ugonjwa wa ebola na kwamba wamegunduliwa katika mji mkuu wa
nchi hiyo Freetown.
Hapo awali ilidhaniwa kwamba mji huo ulikuwa
hauna maambukizi ya ugonjwa huo,na hakukuwa na wagonjwa walioripotiwa
hapo kabla kwa muda wa wiki kadhaa.Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwasababu vituo vyote vya karantini na vitendea kazi vyake vilikuwa vimefungwa mjini Freetown.
Na akaongeza kusema kwamba kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.
Nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.
0 comments:
Post a Comment