Mapigano makali yaendelea Mogadishu
Mapigano makubwa yameripotiwa kwenye
 mji kuu wa Somalia Mogadishu baada ya shambulizi la gari la kujitoa 
mhanga kutokea karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo.
Maafisa
 nchini Somalia wanasema kuwa wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab 
waliingia jengo lililo karibu na makao hayo makuu ya ujasusi, na kukana 
madai ya al-Shabab kuwa waliingia makao ya ujasusi yenyewe.Hakuna ripoti zozote zilizotolewa za watu kuuawa au kujeruhiwa
Al-Shabab wameapa kuongeza mashambulzii dhidi ya serikali ya Somalia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan ambao ulianza siku ya Jumatano.
 RSS Feed
 Twitter

10:36 AM
MZM

0 comments:
Post a Comment