Utumizi wa neno ''uhalifu wa chuki''
ili kuelezea mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la watu weusi mjini
Carolina Kusini nchini Marekani umezua mjadala kuhusu ni nini haswa
kinachosababisha mtu kutekeleza ugaidi.
Watu wengi wameonyesha
hasira zao kuhusu vile afisa mkuu wa polisi mjini Charleston
alivyoelezea kisa hicho wakati wa mkutano na vyombo vya habari.Mshukiwa Dylan Roof ,mwanamume mwenye umri wa miaka 21 ameshtumiwa kwa kuingia ndani ya kanisa saa tatu za usiku siku ya jumatano na kuwapiga risasi waumini waliokuwa katika maombi.
0 comments:
Post a Comment