Wanamgambo wamewaua karibu walinda
usalama 15 nchini Somalia baada ya kufanya shambulizi katika mji ulio
karibu na mji mkuu Mogadishu.
Maafisa wanasema kuwa wanamgambo wa
Al Shabaab kwanza walishambulia kizuizi cha polisi cha Afgoye ambapo
waliwaua polisi watatu na kuchukua magari kadha.Kisha waliwavamia na kuwaua wanajeshi kadhaa.
Al Shabaab wanasema kuwa wameongeza mashambulizi siku za hivi majuzi kwa sababu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.
0 comments:
Post a Comment