Mtu aliyekunywa pombe haram akihudumiwa 
                    
Watu wapatao 35 wamekufa katika mji wa Mumbai nchini India baada ya kunywa pombe haramu.
Wengi wao wamelazwa hospitali.
Waziri kiongozi wa jimbo la Maharashtra ametaka ufanyike uchunguzi, watu watatu wamekamatwa.
Pombe
 haramu aina ya gongo inayotokana na mahindi inanyweka kwa kiasi kikubwa
 nchini kote India ambako wakati mwingine pombe hiyo inauzwa chini ya 
dola moja ya Kimarekani, ikisababisha vifo vya mara kwa mara.
Karibu watu 170 wameripotiwa kufa katika jimbo la Bengal baada ya kunywa pombe hiyo maarufu kama "moonshine"
 RSS Feed
 Twitter

5:44 AM
MZM

0 comments:
Post a Comment