Saturday, June 20, 2015

 Majruhi wa ajali ya gari akihudumiwa
Polisi wa Austria wanasema kuwa mtu mmoja aliendesha gari lake kwa kasi na kutumbukia kwenye kundi la watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katikati ya mji wa kale wa Graz, na kuuwa watu watatu.

Wengine kadha walijeruhiwa.
Dereva amekamatwa.
Wakuu wamesema hakuna ishara kwamba lilikuwa shambulio la kigaidi; na inaelekea kuwa mshukiwa alikuwa amechanganyikiwa kwa sababu ya matatizo ya kibinafsi.
Walioshuhudia tukio wanasema waliona gari likipita kwa kasi sana, na wanasema likionekana kuwa likilenga hasa wapita njia.
Idadi kubwa ya magari ya wagonjwa na helikopta zilitumwa huko.

0 comments: