Wednesday, February 10, 2016

 
Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979
Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi,alisema endapo atachaguliwa kuwa rais azimio lake la kwanza itakuwa kuwapatanisha waganda wa kila tabaka na kabila.
Kwa madhumuni hayo anapanga kuwaleta pamoja watu anaohisi kuwa wanaomuunga mkono Idi Amin wale waliomuunga mkono Milton Obote na wale wanaomuunga mkono rasi wa sasa Yoweri Kaguta Museveni.
Viongozi hao watatu ndio waliochangia kwa njia moja au nyengine mwelekeo wa kisiasa wa Uganda.

Amama Mbabazi ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979 utawala ambao ulishuhudia mauaji ya wapinzani wake wengi.
Vilevile anatuhumiwa kwa kuwatimua wahindi wote nchini Uganda kabla ya kupinduliwa na Milton Obote.
Marehemu Idi Amin aliaga dunia akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.
Rais Yoweri Museveni, anatarajiwa kuchaguliwa tena kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa hatamu ya tano.

Chifu Mandla Mandela taabani kwa kuukubali Uislamu 
Hatua ya mjukuu wa kiongozi mwanzilishi wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mandla, 42, kuslimu na kuoa mke wa nne imevutia hisia kali kutoka kwa viongozi wa kabila lake la AbaThembu.
Wazee hao viongozi wenza wa kabila la Mvezo iliyokuwa ya marehemu ya Mandela ''hawaamini kuwa Chifu mzima wa kabila la Mvezo anaweza kuasi tamaduni zake na kuiga zile za mke wake ''
Mandla alifunga ndoa yake ya nne na bi Rabia Clarke katika msikiti mmoja mjini Cape Town Afrika Kusini mwishoni mwa juma.

Rais Magufuli 

Serikali ya Tanzania imebaini wizi wa takribani shilingi milioni 700 sawa na dola laki tatu za marekani ($320,000 )katika shirika lake la Ndege (ATCL) kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Comoro.

Friday, January 29, 2016


Virusi vya HIV
Virusi vya ugonjwa wa ukimwi vinaendelea kujenga kinga dhidi ya dawa za ugonjwa huo zinazotumika kukinga na kukabiliana na ugonjwa huo,utafiti umesema.
Virusi vya HIV vimeanza kuwa na kinga dhidi ya dawa ya Tenovir katika asilimia 60 ya visa vyote miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika kulingana na utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 1998 na 2015.

Friday, January 15, 2016




Baraza la mitiani NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha 2 kwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka jana ambapo wanafunzi 324,068 sawa na 89% kati ya wanafunzi 363,666 waliofanya mtihani wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu.

Tuesday, January 12, 2016

 Simba
Simba huyo alikuwa pia na masharubu ya ziada
Simba wa milimani aliyeuawa katika jimbo la Idaho, nchini Marekani ameshangaza wengi kutokana na hali kwamba alikuwa na meno ya ziada kichwani.
Meno hayo kamili yanachomoza kutoka kwenye paji la uso na kuonekana kama pembe.
Simba huyo aliuawa na wawindaji walioidhinishwa tarehe 30 Desemba.
Idara ya Wanyamapori na Samaki ya Idaho imesema meno hayo huenda ni masalio ya pacha ambaye labda alifariki akiwa tumboni, au labda inatokana na saratani.
Messi
Hii ni mara ya tano Messi kushinda tuzo hiyo
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.
Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%.
Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita.
Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.

Wachezaji wa Arsenal

Droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la Fa imetoka huku timu za ligi kuu ya England zikipangwa na zile za daraja la chini.
Arsenal, ambao ni mabingwa watetezi wao wamepangwa kukipiga na timu ya Burnley, Huku Chelsea wao wataanzia ugenini kwa kucheza na Mshindi wa mchezo kati ya Northampton Town au Mk Dons.
Man City wao watakipiga na mshindi wa mchezo wa Wycombe Wanderers au Aston Villa. Huku majirani zao Man United wao watakipiga na Derby County.
West Ham, wanasubiri mshindi wa mchezo unaowakutanisha Exeter City dhidi ya majogoo wa Anfield Liverpool.
Michezo hii ya raundi ya nne itachezwa January 29 mpaka Februari 1.

Friday, January 1, 2016

Wimbo mpya wa mwanamziki Mwenendox toka Tanzania amemuandikia Risala mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli wimbo huu umetayarishwa katika studio za Sampamba Music zilizopo nchini mkoani Iringa, Tanzania ili kujua ameandika nini ungana nasikuisikiliza.

Monday, December 28, 2015

Samia
Makamu wa rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alihudhuria mkutano huo
Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.
Wito wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi umetolewa baada ya kikao cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar katika afisi kuu za chama Kisiwandui.

Saturday, December 12, 2015

Burundi
Watu zaidi ya 200 wameuawa Burundi tangu kuanza kwa machafuko Aprili
Miili zaidi ya 34 imepatikana katika barabara za mji mkuu wa Burundi huku machafuko yakiendelea.
Mwandishi wa BBC ameona maiti 21 katika mtaa mmoja wa Bujumbura na maafisa wa serikali wamesema kuna miili mingine 13.
Maiti nyingi zinaonekana kuwa za vijana waliouawa kwa kupigwa risasi, baadhi wakiwa wamefungwa mikono yao ikiwa pamoja mgongoni.
Miili hiyo imepatikana siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo matatu ya jeshi.
Hannibal
Hannibal amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani Oman tangu 2012
Mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Hannibal, ameachiliwa huru baada ya kutekwa nyara kwa muda na kundi la wapiganaji, duru za kiusalama zinasema.
Kwenye video iliyoonyeshwa kwenye runinga ya Lebanon, mfanyabiashara huyo alionekana akiitisha habari zaidi kuhusu kutoweka kwa mhubiri mashuhuri wa dhehebu la Washia nchini Lebanon Musa al-Sadr. Al-Sadra alitoweka mwaka 1978. Alionekana kwenye video hiyo akiwa amejeruhiwa machoni.
Aliachiliwa huru katika mji wa Baalbek na kupelekwa mjini Beirut, polisi waliambia shirika la habari la AP.
Hannibal, 40, alipatiwa hifadhi na Oman mwaka 2012.

Friday, December 11, 2015

Tanzania
Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.

Tuesday, December 8, 2015

Jackson
Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood
Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti.
Trump, mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump.

Wednesday, December 2, 2015

 
Polisi wenye silaha wakipiga doria katika eneo palipotokea mauaji hayo.
Polisi nchini Marekani imesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa San Bernadino mashariki mwa Los Angeles.
Polisi mjini humo inasema tukio hilo imetokea kwenye kituo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na inawezekana lilihusisha watu watatu wenye silaha ambao wametoroka kwa gari.
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivyalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya silaha ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya pati iliyoandaliwa na Idara ya Afya.

Saturday, November 28, 2015

Rais wa Uturuki Rcep Tayyip Erdogan ameonyesha kujuta kwamba Uturuki iliidungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wa taifa hilo na Syria,lakini hakuomba msamaha kwa tukio hilo.
Aliuambia mkutano wa hadhara huko Balikesir kwamba alitamani kwamba tukio hilo halingetokea na kwamba halitarudiwa tena.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amekataa kulijadili swala hilo na Erdogan hadi atakapoomba msamaha.
Moscow inapanga kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Uturuki na tayari imeanza kupitia safari za watalii.
Uturuki imewaonya raia wake kutosafiri Urusi kwa dharura.

Saturday, October 31, 2015

FULL-TIME: #LFC defeat Chelsea Football Club 3-1 at Stamford Bridge thanks to a Philippe Coutinho brace and a goal from substitute Christian Benteke.




Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wabunge ambao wataingia Bungeni baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 25, 2015 ni kama ifuatavyo. 
Idadi kubwa ya wabunge hao ni kutoka chama tawala cha CCM, ikifuatiwa na Chadema na CUF na vyama vingine kama NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.
WABUNGE WALIOSHINDA KUPITIA CCM
Jimbo la Busega (Raphael Chegeni), Nyamagana (Stanslaus Mabula), Msalala (Ezekiel Maige), Ngara (Alex Gashaza), Kigamboni (Faustine Ndugulile), Kishapu (Suleiman Nchambi) na Kisarawe (Suleiman Jaffo).
Majimbo mengine ni Bagamoyo (Dk Shukuru Kawamba), Ilemela (Angelina Mabula), Ilala (Mussa Azzan ‘Zungu’), Singida Mjini (Mussa Sima), Same Magharibi (Dk Mathayo David Mathayo), Rungwe (Saul Amon), Mbogwe (Augustino Masele), Chalinze (Ridhiwani Kikwete), Iramba Magharibi (Mwigulu Nchemba) na Hanang (Dk Mary Nagu).
Aidha, majimbo mengine ni Njombe Kaskazini (Joram Hongoli), Dodoma Mjini (Antony Mavunde), Mtama (Nape Nnauye), Babati Vijijini (Jitu Soni), Kahama Mjini (Jumanne Kishimba), Sikonge (George Kakunda), Nzega Mjini (Hussein Bashe), Urambo (Margaret Sitta), Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso) na Geita Mjini (Constantine Kanyasu).
Chama hicho pia kilijipatia ushindi katika majimbo ya Mbeya Vijijini (Oran Njeza), Mafinga Mjini (Cosato Chumi), Kalenga (Godfrey Mgimwa), Isimani (William Lukuvi), Songea Mjini (Leonidas Gama), Mkalama (Allan Kiula), Newala (George Mkuchika), Kavuu (Dk Prudenciana Kikwembe) na Kwimba (Mansoor Shanif).
Mengine ni Bukoba Vijijini (Jason Rweikiza), Nyasa (Stella Manyanya), Kondoa Mjini (Edwin Sanda), Kondoa Vijijini (Dk Kashatu Kijaji), Chemba (Juma Nkamia), Chamwino (Joel Mwaka), Mtera (Livingstone Lusinde), Bahi (Omar Baduel), Mpwapwa (George Lubeleje), Kibakwe (George Simbachawene) na Kongwa (Job Ndugai).
CCM pia imepata Sengerema (William Ngeleja), Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo), Maswa Magharibi (Mshimba Ndaki), Itilima (Njalu Silanga), Bariadi (Andrew Chenge), Meatu (Salum Hamis), Muheza (Balozi Adadi Rajabu), Kasulu Mjini (Daniel Nsanzugwanko), Buhigwe (Albert Ntabaliba), Handeni Vijijini (Mboni Mhita) na Morogoro Mjini (Abdulaziz Abood).
Gairo (Ahmed Shabiby), Rorya (Lameck Airo), Ngorongoro (William Ole Nasha), Mvomero (Suleiman Murad), Morogoro Kusini Mashariki (Mgumba Omary), Morogoro Kusini (Prosper Mbena), Nkasi Kusini (Deuderius Mipata), Nkasi Kaskazini (Ally Keissy), Singida Kaskazini (Lazaro Nyalandu), Singida Magharibi (Elibariki Kingu) na Igunga (Dk Dalaly Kafumu).
Mengine yaliyoenda CCM ni Solwa (Ahmed Salum), Katavi (Issac Kamwele), Mpanda Mjini (Sebastian Kapufi), Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso), Nsimbo (Richard Mbogo), Ruangwa (Kassim Majaliwa), Sumbawanga Mjini (Aeshi Hilaly), Kyela (Dk Harrison Mwakyembe), Ileje (Janeth Mbene) na Mbarali (Pirmohamed Mulla).
Majimbo mengine yaliyochukuliwa na chama hicho ni Busokelo (Atupele Mwakibete), Vwawa (Japhet Hasunga), Lupa (Victor Mwambalaswa), Songwe (Philipo Mulugo), Madaba (Joseph Mhagama), Peramiho (Jenista Mhagama), Kilosa Kati (Mohamed Bawazir), Kiteto (Emanuel Papian), Mbulu (Paul Isaay) na Karagwe (Innocent Bashungwa).
Kyerwa (Innocent Bilakwate), Nkenge (Dk Diodorus Kamala), Muleba Kusini (Profesa Anna Tibaijuka), Muleba Kaskazini (Charles Mwijage), Biharamulo Magharibi (Mukasa Oscar), Mwibara (Kangi Lugola), Bunda Vijijini (Boniphace Getere), Makete (Dk Norman Sigala), Kibaha Vijijini (Hamoud Jumaa) na Sumve (Richard Ndassa).
Magu (Kiswaga Destery), Chato (Dk Merdad Kalemani), Nzega Vijijini (Dk Khamis Kigwangallah), Njombe Mjini (Edward Mwalongo), Mwanga (Profesa Jumanne Maghembe), Nyangh’wale (Hussein Kassu), Newala Vijijini (Rashid Akbal), Butiama (Nimrod Mkono), Korogwe Vijijini (Stephen Ngonyani) na Korogwe Mjini (Mary Chatanda).
Misungwi (Charles Kitwanga), Busanda (Lolensia Bukwimba), Manonga (Seif Gulamali), Tabora Mjini (Emmanuel Mwakasaka), Mlalo (Rashid Shangazi), Kisesa (Luhaga Mpina), Lindi Mjini (Selemani Kaunje), Mkinga (Dustan Kitandula), Mbinga Mjini (Sixtus Mapunda), Mbinga Vijijini (Martin Msuha) na Musoma Mjini (Vedastus Mathayo).
Mengine ni Geita Vijijini (Joseph Kasheku), Kibaha Mjini (Silvestry Koka), Bukombe (Dotto Biteko), Shinyanga Mjini (Steven Masele), Msalala (Ezekiel Maige), Pangani (Jumaa Aweso), Mufindi Kaskazini (Mahamoud Mgimwa), Mufindi Kusini (Mendrad Kigola), Kilolo (Venance Mwamoto) na Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo).
Maswa Magharibi (Mashimba Ndaki), Chilonwa (Joel Mwaka), Mtwara Vijijini (Hawa Ghasia), Nanyamba (Abdallah Chikota), Tunduru Kusini (Daimu Mpakate), Tunduru Kaskazini (Ramo Makani), Bunda Vijijini (Boniface Mgetere), Mkuranga (Abdallah Ulega) na Mbulu Vijijini (Gregory Massay) nayo yameenda CCM.
Mengine ni Mbulu Mjini (Zacharia Paul), Kilindi (Kigua Mohamed), Namtumbo (Edwin Ngonyani), Ushetu (Elias Kuandikwa), Bumbuli (January Makamba), Segerea (Bonnah Kaluwa), Kalambo (Josephat Kandege), Wanging’ombe (Gerson Lwenge), Kigoma Kaskazini (Peter Serukamba), Muhambwe (Justus Nditiye), Kasulu Vijijini (Agustie Vuma) na Kilolo (Venance Mwamoto).
WABUNGE WA CHADEMA
Kwa upande wa CHADEMA, hadi sasa kimejinyakulia majimbo 35 ambayo ni Kibamba (John Mnyika), Mikumi (Joseph Haule), Bukoba Mjini (Wilfred Lwakatare), Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka), Rombo (Joseph Selasini), Bunda Mjini (Ester Bulaya), Hai (Freeman Mbowe) na Mbeya Mjini (Joseph Mbilinyi).
Majimbo mengine ni Kawe (Halima James Mdee), Longido (Onesmo Nangole), Ukonga (Waitara Mwita), Mlimba (Suzan Kiwanga), Singida Mashariki (Tundu Lissu), Ubungo (Said Kubenea), Mbozi (Paschal Haonga), Tunduma (Frank Mwakajoka), Momba (David Silinde), Kilombero (Peter Lijualikali) na Karatu (Willy Qambalo).
Aidha, chama hicho kilishinda katika majimbo ya Simanjiro (James ole Millya), Arumeru Magharibi (Gipson ole Meseyeki), Tarime Mjini (Ester Matiko), Siha (Godwin Mollel), Buyungu (Kasuku Bilago), Monduli (Julius Kalanga), Arumeru Mashariki (Joshua Nassari), Serengeti (Marwa Ryoba) na Babati Mjini (Pauline Gekul).
Mengine ni Moshi Mjini (Jaffar Michael), Tarime Vijijini (John Heche), Iringa Mjini (Peter Msigwa), Ndanda (Cecil Mwambe) na Moshi Vijijini (Anthony Komu). CUF yenyewe hadi sasa kina majimbo 17 ambayo ni Temeke (Abdallah Mtolea), Mchinga (Hamidu Bobali), Kilwa Kusini (Said Bungala), Kaliua (Magdalena Sakaya), Tandahimba (Ahmad Katani), Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma), Kinondoni (Maulid Mtulia), Kilwa Kaskazini (Vedasto Ngombale) na Tanga Mjini (Musa Mbaruk). Majimbo mengine ni Wawi, Chakechake, Ole, Ziwani, Kojani, Gando, Wete na Mgogono.
WABUNGE WENGINE KUPTIA CHADEMA, CUF, ACT WAZALENDO na NCCR MAGEUZI
Hai(Freeman Mbowe), Vunjo (James Mbatia) Kigoma Mjini (Zitto Kabwe), Arumeru Mashariki (Joshua Nassari), Kawe (Halima Mdee), Ukonga (Waitara Mwita), Kibamba (John Mnyika), Ubungo (Said Kubenea), Bunda Mjini (Ester Bulaya), Tunduma (Frank Mwakanjoka), Siha (Dk Godwin Mollel), Tarime Vijijini (Esther Matiko), Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka), Kaliua (Magdalena Sakaya), Mlimba (Suzan Kiwanga), Iringa Mjini (Peter Msigwa).
Chanzo: Habari Leo Online

Friday, October 30, 2015


 Msafara wa Bw Magufuli umelindwa vikali na maafisa wa usalama
11:30am: Msafara wa Rais mteule John Magufuli pamoja na ule wa Rais Jakaya Kikwete waelekea ikulu chini ya ulinzi mkali.