Baada mwanamitindo na msanii Jokate kuandika ujumbe mzito kwa Diamond 
Platnumz na kumshutumu kwa kuweka video inayomuonyesha akicheza wimbo wa
 “Mdogomdogo” Diamond alipoongea na 255 ya Clouds Fm alimjibu kwa kusema
 haya.
Diamond amesema “Mimi nimempost kama fan wangu, ile caption yangu 
sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya, ukiona mtu anajishuku ujue 
kuna namna nyuma, mbona mimi napost watu wengi na caption zangu za 
vituko vituko manaake mimi nina caption za vituko mi ni mswahili 
nimezaliwa tandale nimekulia tandale na tandale ndo imenifanya niwe hapa
 nilipo, kuna caption zangu za uswahili coz uswahili ndio umenikuza 
mpaka kuwa fame, mbona naandikaga kwenye caption kwann kwake yeye ndo 
tatizo kwani kuna ubaya gani kuandika mtanyooka tu kama haimuusu,maana 
ukiona hivyo ujue kuna kitu kinamuhusu, yeye mpaka nimeenda kuchukua 
tuzo amesapoti nini, alipost hata post moja ya kusema mpigie kura 
Diamond, anajishaua eti nimesapoti kasapoti nini.”
 RSS Feed
 Twitter

8:22 AM
MZM
 Posted in 
0 comments:
Post a Comment