Hata
baada ya Ubalozi wa Marekani kutanganza kuwa Rais Barack Obama
hakusudii kutembelea eneo alikozaliwa baba yake Kogelo Magharibi mwa
Kenya, bado matarajio ni makubwa miongoni mwa raia.
Kogelo, kijiji
ambacho hakikujulikana hata nchini Kenya zaidi ya miaka kumi iliyopita,
hivi sasa kinatajwa katika magazeti, radio na televisheni kote duniani
kama nyumbani kwa babake rais Barack Obama, Barack Hussein Obama Senior.Makaburi ya babu yake rais Obama, Hussein Onyango Obama na Barack Obama Senior, yamewekwa vigae vipya na tayari kokoto kumwagwa pembeni kuzuia vumbi iwapo wageni watakuja.
Hata tiba inahusiana naObama
Oliver Tambo alieleza masikitiko yake: "Tunamkaribiha Rais Obama huku kwetu.
''Tunamwongojea kwa hamu sana.''
''Lakini tumekasirishwa sana kwa Ikulu ya White House kukataa kumruhusu.''
''Wamruhusu aje nyumbani kwa sababu yeye ni mwana wa hapa kwetu."
Mwingine aliyeudhika ni Peter Malenya, "Ingekuwa bora kama Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye mizizi yake iko hapa Kenya, akifika aende kule Alego kwa asili yake ili amsalimie nyanya yake.''
''Hakuna mtu wa kukupangia wakati unapotaka kotoka kwenu au kumwoa dada yako."
Nyanyake Rais Obama, Mama Sarah Obama, aliniambia kuwa hana shaka kwamba mjukuu wake atafika kwa kuwa walikuwa naye Novemba, mwaka jana katika Ikulu ya White House, ambako aliahidi kuwa atafika nyumbani kijijini.
"Yeye ataingia hapa (Kogelo) kwa sababu.
''Yeye ananipenda sana na anapenda boma hili pia.''
''Lazima atafika hapa kuona kaburi la baba yake," Mama Sarah Obama alinieleza.
Tunapochapisha habari hizi, Ubalozi wa Marekani tayari umesema kuwa ratiba ya Rais Obama haishirikishi kwenda kwake kijiji cha Kogelo lakini bado kuna wale wanaoishi kwa matumaini wanaosema huenda akaenda huko kibinafsi na kwa hivyo kumwona nyanyake sio lazima kuwekwe katika ratiba yake kwa umma.
0 comments:
Post a Comment