Wagombea wawili wa urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka Ujao Uganda wamezuiwa na Polisi katika sehemu tofauti.
Aliyekuwa
waziri mkuu Amama Mbabazi alikamatwa na polisi akiwa mjini Jinja mwendo
wa saa moja kutoka jijini Kampala, akiwa njiani kuelekea mkutano wake
wa kwanza wa hadhara na wafuasi wake mjini Mbale mashariki mwa nchi.Siku ya Jumatano Polisi nchini Uganda walitoa taarifa kusema kuwa bwana Mbabazi hana ruhusa ya kufanya mikutano yoyote ya kisiasa japo alikuwa amewataarifu.
Bwana Mbabazi ananuia kutafuta uteuzi wa chama kinachotawala NRM kuwa mgombea wake rasmi wa Urais katika uchaguzi huo Machi mwaka ujao.
Kwa upande mwingine wa nchi mwansiasa mwingine wa Upinzani Kizza Besigye alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake. Dr. Besigye , ambaye ni kanali mstaafu wa jeshi amewahi kuwania urais wa nchi hiyo mara tatu bila mafanikio.
Alikamatwa akiwa njiani kwenda kwa mkutano wake wa kwanza na wafuasi wa chama chake cha Forum For Democratic Change.
Msaidizi wa Dr Besigye ameambia BBC kuwa mwanasiasa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi karibu na nyumbani kwake. Besigye anashindania kiti hicho cha FDC na aliyekuwa kamanda wa jeshi Gen. Mugisha Muntu.
Dr. Besigye pamoja na bwana Mbabazi wote walikuwa washirika wa karibu zaidi na rais Yowei Museveni ambaye atashindana nao katik auchagzui huo.Museveni amekuwa uongozini kwa miaka thelathini.
Kwa sasa #FreeBesigye inaendelea kutajwa kwa wingi katika mitandao ya kijamii, baada ya watu kugeukia mitandao hiyo kuelezea hisia zao kuhusu kukamtwa kwa wawili hao.
0 comments:
Post a Comment