Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa kuvunja Bunge la 10, mkutano wa 20 wa nchi hiyo.
Hata
hivyo mwandishi wa BBC aliyepo Dodoma, Sammy Awami anaarifu kwamba
wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kinachojumisha baadhi wa
wabunge wa upinzani, wamesema hawatahudhuria ufungaji huo.Mwaka 2010 wakati Rais Kikwete anafungua Bunge hili wabunge wa upinzani walisusia uzinduzi huo pia.
Wabunge hawa walitangaza kususia Bunge hili kutokana na uamuzi wa serikali kuwasilisha miswaada mitatu ya mafuta na gesi kwa hati ya dharura
Pamoja na mambo mengine, Bunge hili litakumbukwa kwa mjadala mkali uliohusu maamuzi ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya TSH Bilioni 200 za akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania
Sakata hili liliwaondoa Mawaziri wawili na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine wa Ikulu na Serikali
0 comments:
Post a Comment