Sunday, July 26, 2015

RAIS WA MAREKANI BARRACK OBAMA AMEKAMILISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI KENYA AMBAPO ALIFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA AKAWAHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA KASARANI NA BAADAYE KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA KIJAMII KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA

16.18pm:Ndege ya rais Obama yaondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta

16.13pm:Rais Obama awasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi na kulakiwa na rais Uhuru Kenyatta tayari kuondoka

16.10pm:Ndege iliombeba rais wa Marekani Barrack Obama imewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi.


15.47pm:Rais Obama amekamilisha ziara yake nchini Kenya na sasa anaelekea nchini Ethiopia kwa ziara ya siku mbili ambako anatarajiwa kuzungumza kuhusu maendeleo ya eneo hili.

15.46pm:Msafara wa rais Uhuru Kenyatta umewasili katika uwanja wa Jomo Kenyatta tayari kumuaga rais Obama aliyewasili nchini siku ya ijumaa.

15.45pm:Matayarisho yote ya kumuaga rais Obama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta yamekamilika huku zulia jekundu likiwekwa.

15.43pm:Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta waonekana ukielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kumuaga rais Obama.

14.55pm:Obama amaliza mkutano wake na makundi ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta.

14.51pm:Tutahakikisha katika mazungumzo yote na serikali kwamba yale yanayozungumzwa yanaangaziwa na iwapo kuna kundi linalokandamizwa basi tutatoa sauti yetu.Viongozi wengi wanapendelea sa na Marekani kuingilia kati wakati hawako katika mamlaka,lakini punde wanapoingia katika mamlaka

14.49pm:Obama:Iwapo kuna sheria ambazo zinatoa fursa kwa jamii kujieleza huchangia ukuwaji wa kimaendeleo.Tutaziangazia sheria zinazojaribu kuwazuia watu wengine kuzungumza.SWala la kigadi halifai kuchukuliwa kuyazima makundi ya kijamii ambayo ni halali.

14.34pm:Sisters Without Borders-Serikali inafaa kuwashirikisha wanawake katika harakati za kukabiliana na utovu wa usalama.Licha ya harakati zetu katika swala hilo serikali bado haijatilia mkazo swala la thuluthi moja ya wanawake katika kila sekta.

14.32pm:SUPKEM-Maafisa wa serikali kama vile walimu wametoroka katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya na hivyobasi kuathiri elimu katika eneo hilo miongoni mwa vijana wengi.

14:29pm:SUPKEM-Viongozi wa Kiislamu pia wameshirikishwa katika kukabiliana na ugadi pamoja na ukandamizaji ikiwemo ukosefu wa vitambulisho kwa vijana wa kiislamu.

14:26pm:SUPKEM-Hassan Olenaado:Tumezungumza na serikali kuhusu kuanza mikutano ya kukabiliana na itikadi kali

14.24pm:Ugaidi:Alilirejelea swala ya kukabiliana na ufisadi,akisema ni muhimu kubadilisha fikira za raia kuhusu vita dhidi ya ugaidi.Amsema kuwa huwezi kukabiliana na ufisadi kwa kutumia nguvu pekee.

14.05pm:Habari njema nchini Kenya ni kwamba kuna katiba mpya ambayo inatoa mwongozo.Baadaye alifungua mjadala wazi katika kikao hicho.

14.02pm:Makundi ya kijamii yalijitokeza baada ya raia kujitokeza na kuanza kuzungumzia maswala yanayowaathiri

13.50pm:Obama awasili katika chuo kikuu cha Kenyatta na sasa anawahutubia viongozi wa makundi ya kijamii

13.00pm:Chuo Kikuu cha Kenyatta Jijini Nairobi

12.42pm:Obama amaliza hotuba yake kwa kusema 'Thank you Asante sana'

12.41pm:Amesema kuwa vijana wamemfanya yeye kujisikia nyumbani.

12.37pm:Ametoa changamoto kwa vijana kuchukua fursa iliopo ili kuiendeleza jamii huku akiongezea kuwa ana hakika kwamba kenya inaelekea katika ufanisi mkubwa

12:35pm:Amewataka wakenya kutokubali kugawanywa katika misingi ya kikabila na kidini.

12:33pm:Amesema kuwa Marekani itashirikiana kwa hali na mali na kenya kukabiliana na tatizo la ugiadi.'Magaidi ni waoga ndio maana hupendelea kutafuta makundi madogo madogo ya kijamii na kujaribu kuyagawanya''.Amesisistiza kuwa ugaid ni sharti ukabiliwe kwa hali yoyote.

12.32pm:Amesema kuwa ni sharti wanawake wapewe nafasi sawa katika jamii.'Udhalilishaji wa wanawake ni utamaduni ambao umekuwa tangu zamani lakini sasa hauna nafasi katika maisha ya sasa .Wanawake na wasichana ni sharti waelemishwa,Amesema kuwa kuna ufanisi mkubwa katika jamii ambayo imewaelemisha wanawake wake.Tuwape wasichana wetu elimu.Tunapowaelimisha wanawake tunawapatia nguvu kuzaa watoto walioelimika.

12.27pm:Amesema kuwa Marekani inashirikiana na Kenya kupitia uwekezaji wa vijana nchini.Amesema kuwa kila taifa lina utamaduni wake,lakini akaongeza kwamba tamaduni nyengine zimepitwa na wakati.Unyanyasaji wa kijinsia ni tamaduni iliopo lakini ni lazima zibadilishwe.zinawarudisha nyuma.

12.25pm:Amasema kuwa harakati za kukabiliana na ufisadi lazima zianze kuanza juu na kwamba sheria za kukabiliana na janga hilo ni sharti ziwekwe,huku akiwataka wananchi kusimama kidete na kukataa ufisadi.

12.23pm:'Ufisadi ndio janga linalozuia mataifa mengi kupiga hatua'.Amesisitiza kuwa iwapo Ufisadi hautakabiliwa vilivyo utaathiri maendeleo ya taifa kwa jumla

12.20pm:'Kwa ushirikiano wetu kuimarika ni sharti tuwe na taasisi zilizo imara katika uongozi wa taifa hili kwa lengo la kuimarisha demokrasia'.Amesema kuwa mara nyengine demokrasia huonekana kupendelea upande mmoja lakini sivyo akasisitiza.Amesema kuwa wanasiasa huwa na misimamo tofauti na hutarajia demokrasia itawapendelea na wasipopendelewa hulalama.

12.17pm:Amesema kuwa Marekani ni mshirika wa karibu na rafiki mkubwa wa Marekani na hivyobasi itaendelea na ushirikiano huo kupitia kuhakikisha kuwa kuna uongozi mzuri nchini Kenya.

12.16pm:Ugaidi ni swala jingine ambalo Obama anasema kuwa limerudisha nyuma maendeleo na kutoa heshima zake kwa wale ambao wamepoteza maisha yao katika kukabiliana na janga hilo pamoja na wale walioathirika.

12.15pm:'Siasa za kikabila na za kibaguzi hazina mwelekeo na hazifai kuendelezwa',alisema Obama

12.14pm:Ufisadi-amesema kuwa unafaa kukabiliwa kwa njia mbali mbali kwa kuwa unawadhulumu wakenya wa kawaida pato lao la kila siku.

12.12pm:Alitoa sifa kwa marehemu Wangari Maathai kwa jitihada zake na ukakamavu wa kupigamnia demokrasia.

12.11pm:Amesema kuwa wakenya walikataa kugawanywa katika misingi ya kikabila huku sauti za viongozi na makundi ya kijamii yakisababisha kupitishwa kwa katiba mpya

12.10pm:Alizungumza kuhusu vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo nusra viangamize taifa la Kenya.

12.09pm:Uwezo wa vijana na maendeleo yaliopigwa na kenya ni fursa nzuri kwa vijana kujiendeleza wakati wowote.

12.06pm:Babu yangu alikuwa mpishi wa wakoloni.Obama alieleza vile alivyoweza kupata elimu.

12.04pm:'katika uwanja wa ndege mwanamke mmoja aliona jina langu na kuniuliza iwapo ninahusiana na Mtu anayemjua kwa jina Barrack Obama,na hapo ndipo nilijua kuwa jina hilo ni muhimu'

12.03pm.Obama anasema kuwa alipozuru kenya kwa mara ya kwanza alikula ugali na sukuma na pia alikuwa akilala katika kiti katika nyumba ya dadaake Auma.

12.03pm:'Nakumbuka nilipokuja miaka 30 iliopita nilipoteza mzigo wangu katika uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta ,lakini hilo haliwezi kufanyika katika Airforce one'.alisema Obama

12.01pm:Obama aingia katika jukwaa na kuwasalimia wakenya Habari zenu,wakenya mupo.Nafurahi kuwa wakenya kwa kuwa rais wa kwanza kutembelea kenya.Na pia kuwa mtu wa kwanza kutoka kenya kuwa rais wa Marekani,.

12.00pm:Auma amkaribisha Obama

11.58am:Amewachekesha wengi aliposema kuwa nduguye Barrack ambaye alimchukua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa gari aina ya Beattle takriban miaka 30 iliopita amerudisha hisani yake alipombeba ndani ya gari la the Beast wakati alipowasili.

11.56am:Auma amewakumbusha wakenya kwamba rais Obama yuko hapa kikazi licha ya kuwa mwana wa kenya.

11.53am:Awahutubia wakenya kuhusu dhifa ya hapo jana ambapo anasema kuwa rais huyo wa Marekani alikula vyakula vya aina mbali mbali vya kienyeji licha ya kukaa Marekani kwa muda mrefu.

11.52am:Dadaake Rais Obama Auma Obama amepanda katika jukwaa kwa sasa

11.30am: Obama-Rais Barrack Obama wa Marekani pia amedaiwa kufika katika maeneo ya uwanja wa kasarani jijini Nairobi na wakati wowote kuanzia sasa atakaribishwa na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta ndani ya Ukumbi huo.

11.25am:Uhuru awasili Ukumbini
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewasili katika ukumbi wa Kasarani


11.10am:Ukumbi wa Kasarani
Ukumbi wa Kasarani ambapo rais Barrack Obama wa Marekani na mwenyeji wake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanapaswa kuwahutubia Wakenya tayari umejaa mamia ya wageni waalikwa wakiwasubiri viongozi hao wawili.Tayari viongozi mbali mbali wakiwemo wale wa Upinzani wamewasili katika eneo hilo.


11.05am:Usalama Kasarani
Usalama umeimarishwa katika uwanja wa Kasarani,ambalo ndio eneo ambalo rais Barrack Obama wa Kenya anatarajiwa kuwahutubia Wakenya

11.01am:Obama akicheza densi
Rais wa marekani Barrack Obama siku ya jumamosi usiku alijiunga na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta katika chakula cha usiku na baadaye kucheza densi katika ikulu ya rais jijini Nairobi.
HABARI YA ASUBUHI -JUMAPILI TAREHE 26-JULY.

0 comments: