Tuesday, September 29, 2015


Kanisa KageraHaijabainika ni nani anayeteketeza makanisa hayo
Makanisa manne yameteketezwa katika mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania na kufikisha saba, idadi ya makanisa yaliyochomwa moto eneo hilo mwezi huu.
Hadi sasa haijabainika ni kundi gani linalohusika na vitendo hivyo, kwa mujibu wa polisi.
Lakini baadhi ya viongozi wa dini wameambia mwandishi wa BBC Leonard Mubali kuwa huenda ni matokeo ya uhasama wa kidini.
Kuchomwa kwa makanisa hayo kumeongeza hofu kwa viongozi wa makanisa na waumini kuhusu usalama wao.

Sunday, September 27, 2015

Naibu spika wa bunge Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la"Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti nya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake

Saturday, September 26, 2015

 
 Mpagi Edward Edmary
Mnamo mwaka 1982 Mpagi Edward Edmary ,dereva wa texi nchini Uganda alipewa hukumu ya kifo kwa mauaji ya kinyama ya jirani yake.
Licha ya Edward kuwa mtu asiye na hatia hakuhukumiwa na mauaji yoyote.
Edward alisingiziwa katika mgogoro wa shamba wa familia.

Saturday, September 19, 2015

 
Rais Barack Obama amemteua Eric Fanning kuwa katibu mpya katika jeshi la Marekani. 
Rais wa Marekani Barack Obama amemteua Eric Fanning kuwa katibu mpya katika jeshi la Marekani.

Friday, September 11, 2015

hii ndio shule ya Sekondari Masimbwe aiko wilayani Ludewa kata mpya ya Lubonde
 Mkuu wa shule ya Masimbwe Mwalimu Eliud Sanga

Tuesday, September 8, 2015


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Monica Laurent (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha msemaji wa mkutano huo kuzungumza na waandishi.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo ninastahili kushiriki uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni.

Wednesday, September 2, 2015

 
Mwanamke mmoja aliyekuwa akitumia choo cha muda, alibebwa na kupelekwa sehemu nyingine wakati choo hicho kilipoinuliwa juu na tracta kimakosa na kuhamishwa hadi eneo lingine.
Mwanamke huyo alikuwa ameenda kutumia choo hicho kabla ya ufunguzi wa tamasha la Newlyn Fish Festival, Cornwall nchini Uingereza.

Saturday, August 29, 2015

 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
 kijiji cha Kikondo kata ya Ilungu Mbeya vijijini akiwa njiani kuelekea mkoa wa Njombe .

Friday, August 28, 2015

 
Wanajeshi wa waasi CAR
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF, limesema kuwa makundi yaliyojihami nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, yamewaachilia watoto mia moja sitini na watatu.
Watoto hao waliachiliwa mjini Batangafo, baada ya majadiliano kati ya shirika hilo na makundi hayo ya waasi mwezi Mei mwaka huu, kama sehemu ya mpango wa amani.
 
Treni
Afisa mmoja wa serikali ya Poland, amesema kuwa ana imani kuwa treni moja ya kijeshi ambayo imefichwa tangu vita vya pili vya dunia, zaidi ya miaka sababini iliyopita, na kusemekana kubeba vitu vya z

Mtu yeyote anapoingia katika maisha huwa anakabiliwa na changamoto ya kuamua kati ya kujiajiri au kuajiriwa. Kuajiriwa kunakuhakikishia usalama kazini japokuwa usalama huo siku hizi ni nadra sana kuwepo, wakati kujiajiri hukuhakimkishia uhuru wa kuamua mambo yako. Watu wengi huamua kuchagua kuajiriwa kwa sababu ni rahisi kuliko kuwa wajasiriamali ambako ni kugumu, tatizo wanalolipata ni kuwa wanaishi kwa kutegemea mshahara ambao huwa hautoshi na kujiingiza kwenye madeni mabaya ambapo hukopa kwa ajili ya matumizi na kuendelea kuwa na madeni makubwa zaidi. Kukopa siyo kubaya ila kuna madeni mabaya na madeni mazuri madeni mabaya ni yale ambayo mtu anakopa kwa ajili ya hela ya kula au kutumia, madeni mazuri ni yale ambayo mtu anakopa kwa ajili ya kuwekeza kwenye vitegauchumi au kwenye biashara kwa kufanya hivyo mtu anaweza kujitoa kwenye matatizo.

Thursday, August 27, 2015


Junaid Hussain
Marekani imesema mpiganaji wa Kiingereza, ambaye alijiunga na kundi la Islamic State ameuawa katika shambulio la anga nchini Syria.
Junaid Hussain ambaye alikuwa akiendesha kampeni za kundi hilo la Islamic State kupitia mitandao ya kijamii na kufanya kazi kubwa kuwavuta na kuwaingiza katika kundi hilo, raia wa kigeni.

Wednesday, August 26, 2015

Akihutubia mamia ya watu waliojaa leo huko sumbawanga

Tuesday, August 18, 2015


Mfanyabiashara tajiri kijana Mohamed Dewji
Mfanyabiashara maarufu nchini na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji (pichani) kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.
Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .
 
Shambulizi la Thailand lalaaniwa
Waziri mkuu wa Thailand ametaja shambulizi la bomu ambalo limewauwa zaidi ya watu ishirini mjini Bangkok hapo jana jumatatu kuwa kisa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Thursday, August 6, 2015





Imesubiriwa kwa shauku iliyoje, mengi yamesemwa lakini imefikia hatua ya mitandao mingi kufanya tukio hili kuwa habari iliyofika kwenye madawati yao hivi punde.
Kwa post hii ya Diamond kwenye ukurasa wake wa Twitter na Instagram dakika chache zilizopita ni dhahiri kuwa familia ya Wasafi imepata ongezeko la mtoto wa kike.

Wednesday, August 5, 2015

 
Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.

Tuesday, August 4, 2015

 NUH & SHISHI
Kuna sauti ambayo imerekodiwa na kinachosikika ni sauti ya mwanamke na mwanaume wakijibizana, waliotajwa kwamba ndio wanaosikika kwenye sauti hiyo ni Nuh Mziwanda na Wema Sepetu, imemfikia Soudy Brown tayari !!
Soudy Brown anasema sauti hiyo ilirekodiwa usiku mmoja kabla ya Tuzo za KTMA, na baada ya ishu kuwafikia wote wawili yani Nuh na mpenzi wake Shilole haijulikani nini kinaendelea kati yao kwa sasa.
Sauti yote iko hapa mtu wangu, ukiplay utawasikia wote ilivyokuwa kwenye U Heard August 03 2015

Monday, July 27, 2015


 
Bobbi Kristina afariki Dunia
Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.

Sunday, July 26, 2015

RAIS WA MAREKANI BARRACK OBAMA AMEKAMILISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI KENYA AMBAPO ALIFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA AKAWAHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA KASARANI NA BAADAYE KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA KIJAMII KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA

16.18pm:Ndege ya rais Obama yaondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta

16.13pm:Rais Obama awasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi na kulakiwa na rais Uhuru Kenyatta tayari kuondoka

16.10pm:Ndege iliombeba rais wa Marekani Barrack Obama imewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi.