Sunday, May 3, 2015

Tarehe May 1, 2015
Pacquiao (kushoto) akiwa na Mayweather na rekodi zaokwa pamoja
Pacquiao (kushoto) akiwa na Mayweather na rekodi zaokwa pamoja
Kuelekea pambano la ndondi la kukata na shoka kati ya Floyd Mayweather Jr dhidi ya Manny Pacquiao ‘Pac Man’ kuna orodha ya mabondia watano ambao kwa nyakati tofauti wamewahi kupambana na Mayweather na Pacquiao.
Na hivi ndivyo namna ambavyo kila mmoja aliwashinda wapinzani hao.
OSCAR DE LA HOYA
Mayweather alishinda, ilikuwa ni mwaka 2007
Pacquiao alishinda, ilikuwa ni mwaka 2008
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mchezo huo wanasema kuwa, Pacquiao alishinda kwa mbinu bora zaidi.
Floyd Mayweather akimchapa konde la maana usoni mpinzani wake Oscar de la Hoya
Floyd Mayweather akimchapa konde la maana usoni mpinzani wake Oscar de la Hoya
Manny Pacquiao akimchakaza pia De La Hoya na kumsababishia kustaafu masumbwi rasmi
Manny Pacquiao akimchakaza pia De La Hoya na kumsababishia kustaafu masumbwi rasmi
RICKY HATTON
Mayweather alishinda kwa Techinical Knock Out mwaka 2007, tarehe 10
Pacquiao alishinda kwa Knock Out tarehe , 2009
Katika hili pambano Pacquiao anapewa faida kwa kushinda kwa ubora zaidi ya Mayweather
Hapa anasema; “Bado narudia kwa kusema kuwa Floyd anatakiwa kujifunza zaidi namna ya kumpiga huyu”, De La Hoya.
Mayweather akipambana na Ricky Hatton
Mayweather akipambana na Ricky Hatton
Pacquiao akionekana kumchakaza Ricky Hatton kiasi cha kupoteza fahamu kabisa katika mzunguko wa pili tu
Pacquiao akionekana kumchakaza Ricky Hatton kiasi cha kupoteza fahamu kabisa katika mzunguko wa pili tu
JUAN MANUEL MARQUEZ
Mayweather alishinda mwaka 2009
Pacquiao alidroo mwaka 2004
Pacquiao alishinda mwaka 2008
Pacquiao alishinda kwa pointi za majaji 2011
Pacquiao alipoteza kwa Knock Out katika raundi ya 6 mwka 2012
Hapa karata imemuangukia Mayweather.
Mayweather akipambana na Manuel Marquez
Mayweather akipambana na Manuel Marquez
Marquez alimpa Pacquiao wakati mgumu sana, lakini alisubiri mpaka pambano la mwisho kati ya mapambano 4 kumshinda Pacquiao
Marquez alimpa Pacquiao wakati mgumu sana, lakini alisubiri mpaka pambano la mwisho kati ya mapambano 4 kumshinda Pacquiao
SHANE MOSLEY
Mayweather alishinda mwaka 2010
Pacquiao alishinda mwaka 2011
Mayweather akimuadhibu Mosley
Mayweather akimuadhibu Mosley
Mosley akipokea kichapo toka kwa Pacquiao
Mosley akipokea kichapo toka kwa Pacquiao
MIGUEL COTTO
Mayweather alishinda mwaka 2012
Pacquiao alishinda mwaka 2009
Mayweather vs Pacquiao: kwenye pambano hili Pacquiao alionekana kushinda kwa mbinu bora zaidi ya Mayweather.
Miguel anasema: “Manny ana kasi na nguvu. Manny yuko bora zaidi ya Mayweather”
Miguel Cotto akimtundika konde Mayweather kabla ya kushindwa katika raundi ya mwisho kabisa ya mchezo
Miguel Cotto akimtundika konde Mayweather kabla ya kushindwa katika raundi ya mwisho kabisa ya mchezo
Pacquiao akizichapa dhidi ya Cotto
Pacquiao akizichapa dhidi ya Cotto

0 comments: