Burundi: rais aonekana akicheza licha ya maandamano
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana akicheza mpira pamoja na
marafiki zake mjini Bujumbura licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.
Rais Nkurunziza ni kocha aliyehitimu
Rais Nkurunziza,alikuwa
akisakata kabumbu ndani ya mji mkuu wa Bujumbura mji uliokumbwa na
maandamano makubwa tangu atangaze nia ya kuwania awamu ya tatu
uongozini.
Hii leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.
Rais Nkurunziza alikuwa akicheza dhidi ya marafiki zake
Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.
Walioshuhudia
wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa
katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.
Mechi hiyo ilikuwa mjini Bujumbura
Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi.
Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na
hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita,
warejee nyumbani.
Rais Nkurunziza anatimu yake ''Hallelujah FC ''
Katika hotuba kwenye runinga ya taifa, amesema kuwa asilimia tisini na tisa nukta tisa ya Burundi ina amani.
Anasema kuwa hakuna mtu yeyote anayetaka kufufua taharuki ya kikabila.
0 comments:
Post a Comment